Wakati unaendelea kujijengea tabia ya kujiamini ni muhimu kujua kwamba mambo unayofanya kila siku yanaweza kuwa yanakujengea kujiamini zaidi au yanabomoa kujiamini kwako. Leo tutajifunza mambo au tabia ambazo kama unapenda kuzifanya zinaweza kuwa zinakuongezea kujiamini au zinaondoa kujiamini.

Mambo au tabia ambazo yatakujengea kujiamini.

1. Kuwa na mtu mzuri ambaye unatamani kuwa kama yeye(role medel)

2. Kusifiwa.

3. Kuweka mkazo kwenye mambo chanya.

4. Kuacha kuwakatisha tamaa wengine.

5. Kuweka malengo na kuyafikia.

6. Kufanya mazoezi.

7. Kujisamehe kwa makosa yaliyopita.

8. Kuendeleza ujuzi wako na vipaji vyako.

9. Kujifunza vitu vipya.

10. Kupata muda wa kupumzika.

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo ukiyafanya utajiongezea kujiamini. Yafanye mambo haya mara kwa mara na utaongeza kujiamini kwako.

Mambo au tabia ambazo zinakuondolea kujiamini.

1. Kujilinganisha na wengine.

2. Kuwa na watu hasi ambao unataka kuwa kama wao(role model)

3. Kujishusha na kujiona wa chini.

4. Kuweka mkazo na kuwa na mawazo hasi.

5. Kukatishwa tamaa na wengine hasa watu wa karibu.

6. Kudharau uwezo wako wa ndani.

7. Kutegemea kuwa mkamilifu.

8. Kushindwa kila mara.

9. Kuvunjia kwa mahusiano uliyokuwa nayo.

10. Kukosa mlo kamili, kukosa mazoezi na kukosa muda wa kupumzika.

Mambo hayo yanakuondolea kujiamini binafsi, hivyo yaepuke au acha kabisa kuyafanya.

Hayo ndio mambo ambayo ukiyafanya yanaweza kukujengea au kukuondolea kujiamini. Anza kuyafanyia kazi ili uendelee kujijengea tabia ya kujiamini.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA.