Tunaendelea na uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON.
Ukipewa mfuko uliojaa fedha na kitabu chenye maneno ya busara utachagua nini? Hili ni swali ambalo liliulizwa na Kalabab kwa watu 27 waliokuwa kwenye mjadala. Watu wote walijibu watachukua mfuko wa fedha.
Kalabab alishangaa na kuendelea kusema, sikia mbwa mwitu wakibweka usiku ni kwa sababu ya njaa. Ila hata wanapopewa chakula huishia kugombana na kupigania chakula hicho bila ya kujali nini maisha yatakuwaje siku zinazokuja. Alisema hivyo ndivyo ilivyo kwa binadamu. Wape fedha au busara watapuuza busara na watapoteza fedha waliyochagua na baadae kuanza kujutia kwa sababu hawana tena fedha na hata busara hawana.
Aliwaambia fedha zipo kwa wale ambao wanajua sheria zake na kuzitii. Kalabab alikaa vizuri na kuwaambia watu wale kwa sababu wamefanya nae kazi vizuri usiku huo angewapa hadithi nzuri kuhusiana na sheria tano za fedha. Aliwaambia wasikilize kwa makini maneno anayowaambia na kama watayatumia siki zijazo watakuwa na fedha nyingi sana.
Aliwaambia jioni hiyo angewaambia kuhusu buasara za Arkad ambaye alikuwa mtu tajiri kuliko wote babeli. Aliwaambia alikuwa mtu tajiri kwa sababu alikuwa na busara na alielewa vizuri sheria za fedha. Aliwaambia usiku huo angewapa hadithi ya busara zake kama alivyoambiwa na mtoto wa Arkad aliyekuwa anaitwa Nomasir.
Wakati huo wa babeli ilikuwa kawaida kwa mtoto wa tajiri kukaa na wazazi wake akitegemea kuridhi mali hizo za wazazi wake. Arkad hakukubaliana na utaratibu huu. Hivyo mwanae Nomasir alipofikia umri wa mtu mzima alimwita na kumwambia maneno yafutatayo “Mwanangu natamani sana urithi mali zangu, ila nataka kwanza uoneshe kwamba unaweza kuziendeleza, hivyo nakutuma uende duniani na uoneshe uwezo wa kupata fedha na pia kuheshimika mbele za watu. Kwa kuanzia nitakupa vitu viwili, kwanza nitakupa mfuko wa fedha, kama utazitumia vizuri utakuwa msingi wa utajiri wako. Pili nakupa kitabu chenye sheria tano za fedha, kama ukizisoma na kuzitumia zitakuwezesha kufikia mafanikio.
Aliendelea kumwambia miaka kumi ijayo kuanzia leo, urudi kwenye nyumba ya baba yako na ueleze ni jinsi gani umeweza kutumia vitu nilivyokupa. Kama utakuwa umepata mafanikio nitakupa mali zangu uzirithi na kama utakuwa huna mafanikio mali zangu nitawapa wahubiri ili waniombee vizuri.
Nomasir aliondoka na fedha zake na kitabu cha sheria, alisaidiwa na watumwa wake na pia walikuwa na farasi wa kusafiria.
Miaka kumi ilipita na Nomasir alirejea nyumbani. Baba yake alifanya sherehe kubwa na kuwaalika marafiki zake. Na baada ya shamra shamra Nomasir alisimama mbele ya watu wale na kuanza kueleza jinsi alivyoweza kutumia vitu vile viwili alivyopewa na baba yake.
Alianza kwa kumshukuru baba yake na kusema kwamba alimpa uhuru wa fedha na uhuru wa busara. Alisema kwa fedha alipata changamoto kubwa sana kwa kushindwa kuzitumia vizuri. Aliendelea kusema alipopewa vitu vile aliamua kwenda eneo linaloitwa Nineveh akiamini kwamba huko angekutana na fursa. Aliungana na msafara wa watu wengine waliokuwa wakisafiri kuelekea huko. Katika safari hiyo watu wale walimwambia kwamba kuna tajiri mmoja wa Nineveh ambaye ana farasi ambaye hajawahi kushindwa kwenye mashindano yoyote. Ila walimwambia farasi yule hana uwezo mkubwa hivyo kama yuko tayari aweke fedha na watatoa farasi mzuri atakayemshinda farasi yule na watapata fedha zilizowekwa na tajiri yule. Nomasir alifanya hivyo ila farasi wa tajiri yule alishinda na akapoteza fedha zake, baadae alikuja kugundua kwamba ule ulikuwa mchezo wa watu wale kwa kila anayeingia Nineveh. Alisema tukio hilo lilimpa funzo la kwanza ambalo lilikuwa kujiangalia kwanza.
Katika safari ile alikutana na mtu mwingine ambaye walijenga urafiki. Mtu huyu naye alikuwa mtoto wa tajiri ambaye naye alienda kujifunza kuhusu fedha na maisha. Walipofika Nineveh mtu yule alimwambia kwamba kuna mfanyabiashara amefariki na hivyo biashara yake inauzwa kwa bei rahisi. Alimwambia washirikiane kwenye biashara hiyo, ila yeye atarudi babeli kutafuta fedha na hivyo anunue biashara ile kwa fedha zake na akirudi wataiendeleza. Nomasir alinunua biashara ile ila aliishia kupata hasara.
Baada ya matukio haya Nomasir alikuwa maepoteza fedha zote alizopewa na baba yake na hivyo ilimbidi kutafuta ajira. Kwa bahati mbaya hakuweza kupata ajira kwa sababu hakuwa na ujuzi wowote au utaalamu wa biashara. Hivyo aliuza watumwa wake na hata farasi wake na vingine alivyomiliki ili kuweza kupata chakula. Aliendelea kusema ni katika kipindi hiki kigumu alikumbuka sheria zile alizopewa na baba yake. Alizisoma sheria zile kwa makini na kugundua kwamba kama angezisoma mwanzo kabla ya kuanz akutumia fedha zile asingepata hasara aliyoipata.
Alisema kwa faida ya watu mliohudhuria hapa nitazisoma sheria hizo tano za fedha nilizopewa na baba yangu.
Sheria tano za fedha.
1. Fedha huja na kuongezeka kwa mtu ambaye anaweka pembeni sio chini ya sehemu ya kumi ya kipato chake kama akiba.
2. Fedha hufanya kazi kwa bidii kwa mtu mwenye akili anayeweza kuiwekeza sehemu inayozalisha.
3. Fedha huendelea kubaki kwa mtu anayeilinda na kuiwekeza kwa kufuata ushauri wa watu wenye busara.
4. Fedha hukimbia kwa mtu ambaye anaiwekeza kwenye eneo ambalo halijui au hafuati ushauri wa watu wenye busara.
5. Fedha hukimbia kwa mtu ambaye anailazimisha izalishe sehemu ambayo haiwezi kuzalisha au anayefuata ushauri wa watu matapeli.
Nomasir alisema hizi ndio sheria tano za fedha nilizopewa na baba yangu na nakiri kwamba zina thamani kubwa kuliko fedha yenyewe. Aliwaambia atawaonesha thamani hiyo kutokan na hadithi yake.
Tutaendelea na sehemu ya pili ya uchambuzi huu kwenye makala ijayo.
Tushirikishe ni vitu gani vitano umejifunza kutokana na sehemu hii ya ushambuzi kwenye maoni hapo chini.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia uhuru wa kifedha.
TUPO PAMOJA.
Nimejifunza mengi lakini kubwa na muhimu zaidi kujua ni kwamba pesa ni matokeo tu lakini msingi wake mkuu ni maarifa, kuzijua kanuni zake, na huo ndo mtaji thabiti/imara kuliko aina zingine za mitaji.
LikeLike
Ni kweli kabisa Ibrahim, na ndio maana ni muhimu sana kupata maarifa zaidi ili yatuwezesha kutumia fedha zetu kwa busara na kuweza kuzalisha nyingi zaidi.
LikeLike
Nimejifunza kuwa 1:Fedha zinaweza kutumiwa vizuri pale ambapo mtu ana busara na uelewa,tofauti na hapo ni kujipoteza. 2:Kupata elimu ya kutengeneza fedha ni bora kuliko kupewa fedha yenyewe. 3:Ni muhimu sana kuijali kesho yako kwa kufanya uwekezaji binafsi siku Leo. 4:Fedha zinafanya kazi kwa sheria,ni heri kujifunza sheria hizo ili kufanya fedha zikufanyie kazi kwa bidii sana na kufikia uhuru wa kifedha.5:Kubali huna uelewa/elimu juu ya fedha na kuchukua ya kuwafuata wenye uelewa ama wakufundishe na kufanyia kazi mafunzo yao.
LikeLike
Vizuri sana Ngutiti,
Fanyia kazi mambo haya na utaona mabadiliko makubwa.
LikeLike
1.Watu hupenda fedha kabla ya busara na kujikuta wakipoteza fedha
2.watu hukimbilia maeneo wasiyoyajua na kuwekeza bila kuomba ushauri kwa wenye hekima hivyo hupoteza kila kitu
3.Watu hupenda njia za mkato za kupata UTAJIRI bila kujua kanuni na sheria za UTAJIRI wanazopaswa kuzifuata
4.Fedha hufuata watu wenye busara ya kuzitumia na kuzifanya ziwazalishie
5.Fedha hukimbia watu wenye tamaa wasio na busara na wasiozijua sheria na kanuni za fedha
LikeLike
Vizuri sana Daniel,
Mambo haya yamewafanya watu wengi sana kupoteza fedha nyingi na kuendelea kuwa masikini.
Tujiepishe nayo na tujifunze zaidi.
LikeLike
1.Ni Mara nyingi sijawekeza fedha Katika sehemu inayozaa, hili limeniumiza kwa muda Sasa
2.Kuweka akiba sehemu ya kipato angalau asilimia 10 kumenipa kuinuka tena hata pale napitia anguko la kifedha.
LikeLike
Vizuri kwa kuweza hilo la akiba.
Sasa jiimarishe kwenye hilo la uwekezaji.
LikeLike