Fanya Hesabu Hii Rahisi Ambayo Italeta Ukombozi Kwenye Maisha Yako.

Unahitaji ukombozi kwenye maisha yako. Nasema hivi kwa sababu sehemu kubwa ya watu wanajikuta kwenye kifungo au utumwa ambao hawaujui umewafikaje. Sehemu ya kwanza ya utumwa huu ni ajira na sehemu ya pili ni baadhi ya biashara. Unaweza kuwa kwenye sehemu moja kati ya hizo. Leo tutafanya hesabu moja rahisi sana ambayo itakuletea ukombozi mkubwa kwenye maisha yako.

Hesabu hii ni rahisi sana, hivyo hata kama uliziogopa hesabu shuleni usikimbie hapa maana ni rahisi kama hesabu za fedha ambazo kila mtu anazijua. Na utakaofanya hesabu hii na kisha kutafakari kwa kina utapata majibu mazuri ya kukutoa kwenye kifungo au utumwa uliopo.

Hebu fikiri ni mara ngapi umekuwa ukisema utaondoka kwenye ajira kwa sababu imekuchosa, huipendi na kipato hakitoshelezi mahitaji yako? Je umeweza kutimiza malengo yako hayo? Mpaka sasa unashindwa kutekeleza malengo hayo kwa sababu hujafanya hesabu hii rahisi ya kukusaidia kuondoka kwenye kazi hiyo.

Kufanya hesabu hii chukua kalamu na karatasi au ukiwa na kitabu ambacho huwa unaandika malengo na mipango yako itakuwa vizuri zaidi. Katika kitabu hiko andika idadi ya watu ambao wanaweza kuathiri maisha yako moja kwa moja kiuchumi. Kama umeajiriwa na hivyo kipato chako ni mshahara tu basi mwajiri wako anaweza kuathiri maisha yako moja kwa moja na hivyo mtu mmoja tu anaweza kuathiri maisha yako kwa kiasi kikubwa. Kama unafanya biashara andika idadi ya wateja wa biashara yako. Kama biashara yako ina mteja mmoja mkubwa basi mteja huyo anaweza kuathiri maisha yako moja kwa moja.

KUCHOKA2

Nini lengo la hesabu hii?

1. Jinsi ambavyo watu wachache wanaweza kuathiri maisha yako kiuchumi moja kwa moja ndivyo ambavyo unakuwa mtumwa. Kwa mfano kama umeajiriwa na hicho ndio chanzo pekee cha kipato chako kuna wakati utajikuta unamsujudu mwajiri wako kwa kuwa unajua akikufukuza kazi leo maisha yatakuwa magumu sana. Sawa unaweza kusema una taaluma nzuri hivyo akikufukuza utapata kwingine ila kwa dunia ya sasa soko la ajira limechafuka sana hivyo sio rahisi kufukuzwa kazi leo na siku chahce baadae ukawa tayari umeajiriwa sehemu nyingine.

Kama unafanya biashara na mteja wako ni mmoja, unaweza kujikuta inabidi ukubaliane na mteja huyo hata pale anapokwenda kinyume na matakwa yako kwa sababu akiacha kufanya biashara na wewe utakuwa kwenye wakati mgumu sana.

Soma; Hesabu rahisi za ajira ambazo hutaki kuzikokotoa.

2. Jinsi unavyokuwa na watu wengi ambao wanaweza kuathiri maisha yako kiuchumi ndivyo unavyozidi kupata uhuru au ukombozi. Kwa mfano kama unafanya biashara na una wateja 100, hata wateja 10 wakiamua kuacha kufanya biashara na wewe bado una wateja 90 ambao watakuwa wanaendelea kukupatia kipato huku ukiendelea kutafuta wateja wengi zaidi. Huu ni uhuru mkubwa sana ambao kila mtu anauhitaji.

Ufanye nini baada ya hesabu hii?

Kama umeshafanya hesabu hii na kupata majibu ambayo sio mazuri, yaani unajiona upo kwenye utumwa, hakuna kilichobaki zaidi ya kufanya mabadiliko. Usisema huwezi kufanya mabadiliko yoyote, unaweza vizuri sana sema hujaamua kufikiria ni nini ufanye ili uweze kupunguza utumwa huo.

Hapa nitakushauri mambo manne muhimu unayoweza kufanya ili kuondokana na utumwa huo.

1. Kama unafanya biashara na una wateja wachache au mmoja anza kutafuta wateja wengi zaidi. Mteja mmoja au wachache watakusumbua sana na kukufanya uwe kama mfanyakazi wao au mtumwa wao.

2. Kama umeajiriwa na huna muda wa kufanya biashara unaweza kuanza kukuza biashara ambayo inahusiana na kazi unayofanya. Mara nyingi biashara hii inaweza kuwa huduma za ushauri(consultancy) au huduma nyingine za kitaalamu. Fikiria kwa kina ni kitu gani unaweza kuanza sasa ambacho kinahusiana na kazi unayofanya na kinaweza kukuingizia japo kipato kidogo. Umiza akili yako na itakuletea majibu mazuri sana.

3. Ingia kwenye biashara ambazo hazihitaji muda wako mwingi.

Kuna baadhi ya biashara ambazo hazihitaji muda wako mwingi kuziendesha na kuzisimamia. Pia hazihitaji mtaji mkubwa kuanza au kufanya taratibu nyingi za usajili, kufungua ofisi, leseni na kadhalika. Biashara hizi zinaweza kuwa nzuri sana kwako wewe ambaye umeajiriwa na huna muda wa kufanya kitu kikubwa. Mfano wa biashara hizi ni biashara za mtandao(Network marketing), ukichagua moja na kuifanya kwa bidii baada ya muda utajikuta una kipato kikubwa na hivyo kuanza kupata uhuru.

4. Unaweza kutumia fursa ya kutengeneza fedha kupitia mtandao wa intaneti. Hii ni njia nzuri na rahisi unayoweza kutumia kutengeneza kipato. Uzuri wa mtandao ni kwamba unaweza kuchagua muda utakaofanya kazi na sehemu gani ufanyie kazi na hivyo kutokuingilia ratiba zako za kazi au biashara nyingine. Unaweza kuanza biashara hii kwa mtaji kidogo sana na kama ukiweka juhudi na maarifa utaona matunda mazuri ya biashara yako na hivyo kupata uhuru. Unafanya biashara hii kwa kuwa na blog ambayo ambapo utachagua kitu kimoja utakachokifanya kwa kupitia blog hiyo. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu biashara hii kwenye kitabu jinsi ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog (bonyeza hayo maandishi kukipata). Na kama utakuwa unahitaji kupata ushauri zaidi au kutengenezewa blog tuma ujumbe kwenye email amakirita@gmail.com

Hiyo ndio hesabu muhimu uliyoifanya kwenye maisha yako na hayo ni baadhi ya mapendekezo unayoweza kuanza kuyafanyia kazi. Anza kuyafanyia kazi sasa hivi, sio leo au kesho, mara nyingi kesho huwa haifiki, yafanyie kazi sasa na utaona mabadiliko kwenye maisha yako.

Mabadiliko haya yatachukua muda ndio uweze kuyaona hasa kwenye kipato. Hivyo kama unategemea uanze kufanya kati ya hayo niliyoshauri hapo juu na uanze kupata mapesa haraka sana umekosea sana. Kuwa mvumilivu(kama ulivyovumilia ajira yako mpaka sasa) na fanya kazi kwa bidii na maarifa katika kitu ambacho umechagua kukifanya kwa pembeni.

Nakutakia kila la kheri katika kutafuta ukombozi wa maisha yako.

TUPO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI.

kitabu-kava-tangazo4323

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: