Sasa Ni Muda Wa Wewe Kuchukua Hatua, Usipofanya Leo, Hutofanya Milele.

Haijalishi unaishi wapi, haijalishi umeanzia wapi na haijalishi dini yako au kabila lako, kuna kitu kimoja ambacho kiko sawa kwa watu wote, MAFANIKIO YAPO KWENYE MIKONO YAKO MWENYEWE.

Yaani pamoja na yote unayopitia, wewe ndio utakayeamua kama unataka kufanikiwa au la. Hata ungepewa mazingira mazuri kiasi gani na ukapewa kila kitu unachohitaji, kama usipoamua kutoka ndani yako kwamba unataka kufanikiwa huwezi kufanikiwa.

NJIA YA MAFANIKIO

Unaweza kujishawishi kwamba kama ungeanzia kwenye msingi mzuri ingekuwa rahisi kwako kufikia mafanikio, unaweza kujishawishi kwamba kama ungekuwa na kazi bora leo usingekuwa kwenye matatizo yoyote. Yote haya unajishawishi ili tu kuepuka ukweli kwamba mafanikio yapo kwenye mikono yako na ni maamuzi yako binafsi.

Kila mtu anao uwezo wa kufikia mafanikio makubwa. Lakini atafikia mafanikio hayo makubwa kama ataamua kweli kuyafikia.

Kama ni rahisi hivi kwa nini watu wengi hawajafanikiwa?

Ukweli ni kwamba njia ya mafanikio sio njia iliyonyooka. Ni njia yenye kona na vikwazo vingi na kila mara inashawishi kupumzika au kuachana kabisa na safari hiyo. Ndio maana wanaweza kuanza biashara watu wengi lakini wachache sana ndio wanaofikia mafanikio makubwa. Vile vile watu wengi wanatamani kufanikiwa lakini wachache ndio wanaofikia mafanikio hayo.

Pamoja na kwamba umeamua kuanza safari ya mafanikio unahitaji mazingira ambayo yatakusaidia usikate tamaa. Unahitaji mazingira ambayo yatakutia moyo na kukuonesha njia pale mambo yanapokuwa magumu.

Katika jamii zetu hakuna mazingira hayo, katika kazi zetu hakuna mazingira hayo. Huku kumejaa mazingira ya kukatishana tamaa na kushawishiana kuenda na maisha kama yanavyowapeleka watu.

Utapata wapi mazingira haya mazuri?

Kama kweli umejitoa kufikia mafanikio makubwa na kama kweli umeamua kuachana na sababu zote ambazo umekuwa ukijidanganya kwamba zinakuzuia kufikia mafanikio, kuna mazingira mazuri sana ya wewe kuweza kufikia mafanikio.

Maringira hayo yanapatikna kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kupitia KISIMA utajifunza kuhusu biashara na ujasiriamali, utajifunza kujijengea tabia za mafanikio na kuondokana na tabia zinazokurudisha nyuma. Utapata uchambuzi wa vitabu vizuri ambavyo vitakuongezea maarifa na kukuhamasisha na pia utajifunza mbinu za kuweza kufikia mafanikio makubwa sana.

Kuwepo kwenye KISIMA CHA MAARIFA pia kuakupa nafasi ya kuwa kwenye kundi la WHATSAPP ambapo unakutana na watu wenye mtizamo chanya na waliojitoa kufikia mafanikio na wasiokubali kuzuiwa na kitu chochote. Kupitia kundi hili utapata mijadala mbalimbali ambayo inakuongezea maarifa na kukuhamasisha. Pia mijadala hii itakuonesha fursa mbalimbali unazoweza kuzitumia na ukabadili kabisa maisha yako.

Yote hayo utayapata kwa gharama ya tsh elfu hamsini kwa mwaka, sawa na shilingi 4200 kwa mwezi au shilingi 140 kwa siku. Hii ni fursa kubwa sana ya wewe kujiweka kwenye mazingira ya kufikia mafanikio.

Hela hiyo ni kubwa sana siwezi kuipata!

Huenda hiki ndio kikwazo chako cha kwanza kwamba huwezi kujiunga na KISIMA kwa sababu elfu hamsini ni kubwa sana kwako na huwezi kuimudu. Sawa naweza kukubaliana na wewe kwamba fedha hiyo ni kubwa kwako na sababu kubwa inayokufanya usiweze kuimudu ni kwa sababu hujapata elimu hii muhimu utakayokwenda kuipata kwenye KISIMA.

Hivyo kama huna fedha hiyo, wewe ndio mtu wa kwanza kabisa unayetakiwa kujiunga na KISIMA ili ujifunze kujijengea tabia ya kutunza fedha zako na kuweza kuzizalisha zaidi. Hivyo kwa njia yoyote ile(isipokuwa kuiba), tafuta fedha hiyo ili uweze kujiunga. Iwe utakopa, utaomba au utauza vitu ambavyo huvitumii, fanya kitu leo ili uweze kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA, unakosa mambo mengi na mazuri.

Kama bado elfu 50 inakushinda unaweza kuanza na uanachama wa elfu 10 kwa mwaka au uanachama wa elfu 30 kwa mwaka na ukaendelea kuongeza fedha ili kufikia uanachama wa juu ambapo utapata kila kitu.

Usiendelee tena kukosa nafasi hii nzuri ya kubadili maisha yako.

Kama nilivyosema, uamuzi upo kwako wewe binafsi, ni kama uchukue hatua sasa na uanze kufurahia mabadiliko au uendelee kuishi maisha hayo ambayo huyafurahii na kuendelea kulalamika. Hakuna anayeweza kukushikia bakora, ni uamuzi wa kufanya wewe mwenyewe.

Fanya maamuzi sasa na yasimamie maamuzi yako bonyeza maandishi haya kujaza fomu ya kujiunga na kisima cha maarifa na tuma fedha ya uanachama kwa namba 0717396253/0755953887 baada ya hapo uanachama wako utadhibitishwa na utaanza kupata maarifa yatakayofungua macho yako na kuona tofauti na ulivyokuwa unaona hapo awali.

Nakukaribisha sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, chukua hatua leo ili tuwe pamoja kweye safari hii ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA.

kitabu-kava-tangazo4323

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: