Tunaendelea na uchambuzi wa kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON
Katika uchambuzi uliopita tuliona jinsi ambavyo Sharru Nada alivyokuwa akielezea historia yake ya kwanzia alipokuwa mtumwa mpaka kuja muwa mfanya baishara mkubwa. Alikuwa akimweleza mjukuu wa rafiki yake hadithi hii ili kumhamasisha na yeye afanye kazi kwa juhudi ili aweze kufikia mafanikio. Kwenye uchambuzi huo uliopita tuliishia pale ambapo Sharru Nada alikuwa amenunuliwa kama mtumwa.
Sharru Nada alipelekwa nyumbani kwa bwana aliyemnunua na alikuwa akimsaidia kwenye kazi zake. Bwana yule alikuwa akitengeneza mikate na keki. Kazi kubwa ya Sharru ilikuw akuwasha moto, kukanda unga na kufanya maandalizi mengine. Kutokana na kwamba alikuwa amepanga kufanya kazi kw amoyo mmoja Sharru aliomba kufundishwa kutengeneza mkate na akaweza, baadae akamwomba bwana yule amfundishe kutengeneza keki za asali. Alifundishwa pia kutengeneza keki hizo. Baada ya muda mfupi Sharru alikuwa anawez akufanya kazi zote za bwana yule na bwana yule alifurahi sana kwa kupungukiwa na majukumu.
Sharru alianza kufikiria kwamba anahitaji kuanza kutengeneza fedha ili aweze kununua uhuru wake. Alifikiria kwa vile kazi ya kutengenez amikate ilikuwa inaisha mchana basi angeweza kutumia muda wa jioni na kujitengenezea kipato. Alimfata yule bwana na kumweleza mpango wake kwamba anaomba atumie muda wa jioni kujitengenezea kipato na kipato chochote atakachopata watagawana. Alimweleza mpango wake kwamba angepika keki nyingi na jioni angeziuza njiani kwa wapitaji. Yule bwana alikubali mpango ule na Sharru alianza kuuza keki hku faida wakigawana na yule bwana.
Siku ya kwanz aalitengeneza keki zake nzuri na kuanz akuzipitisha barabarani. Alizunguka sana bila ya kupata mtu yeyote wa kununua. Alianz akukata tamaa lakini alijisukuma kuendelea kuita wanunuaji. Baadae alikutana na watu wenye njaa na wakanunua keki zake na baada ya muda zikawa zimeisha. Yule bwana aliyemnunua alifurahishwa sana na mafanikio yale na waligawana faida iliyopatikana. Sharru alifurahi kuanza tena kumiliki fedha zake mwenyewe japo zilikuwa kidogo.
Aliendelea kumueleza kijana yule kwamba aliendelea na biashara hii kila siku na siku moja ndio alikutana na babu yake na huyo kijana. Yeye alikuwa mfanya biashara na alikuwa akitembeza vitu nyumba kwa nyumba. Kila siku alinunua keki kwa Sharru na siku moja alimwambia nazipenda sana keki zako kwa sababu ni tamu. Na pia napenda sana jinsi unavyofanya biashara, kwa moyo huu utafika mbali sana.
Sharru aliendelea na biashara ile na kadiri siku zilivyokuwa zinaenda mfuko wake wa fedha ulikuwa unanenepa. Aliona jinsi ambavyo kazi imekuwa na manufaa kwake. Wakati huo huo yule bwana aliyemnunua alikuwa anatumia fedha anazopata kucheza kamari na hivyo akawa anamtegemea Sharru kila siku akimaliza kuuza ili wagawane faida. Alimhimiza Sharru kuuza zaidi na kutafuta soko kubwa zaidi la keki zake ili waweze kupata faida kubwa.
Sharru aliendelea kumwambia kijana yule kwamba siku moja babu yake na yule kijana alimuuliza kwa nini unafanya kazi sana? Alimweleza historia yake na kwamba anataka kununa uhuru wake. Alimuuliza tena akishakuwa huru atafanya nini? Alimjibu anataka kuwa mfanya biashara. Alimwambia kwamba hata yeye ni mtumwa na ameingia ubia na bwana aliyemnunua. Kijana yule aliposikia kwamba babu yake alikuwa mtumwa alikataa kabisa na kusema babu yake alikuwa tajiri mkubwa sana na hajawahi kuwa mtumwa. Sharru Nada alimjibu kwa kumwambia kwamba babu yake alianzia kwenye utumwa na kama isingekuwa juhudi zake angebaki kwenye utumwa na hakuna ambaye angemjua. Alimsisitiza sana kijana yule kufuata nyayo za babu yake.
Kuanzia pale walianz aurafiki na Sharru alimpa moyo mwenzake kwamba asiogope kuanza mwenyewe pale atakaponunua uhuru wake. Alimpa ushauri huu baada ya kuwa amemwambia kwamba anaona kama akiondoka kwa bwana yule hataweza kufanikiwa mwenyewe kwenye biashara.
Siku moja wakati Sharru anaendelea kuanda aunga wa kutengeneza keki alikuja kuchukuliwa na watu asiowajua na kuambiwa kwamba bwana aliyemnunua ameshindwa kulipa madeni yake na hivyo wanachukua mtumwa wake. Sharru alibeba mfuko wake wa hela na kuondoka na bwana huyo mwingine. Alifikishwa kwenye eneo la kazi ambapo alifanyishwa kazi ngumu sana. Alitafuta mahali pa kufukia mfuko wake wa hela. Alifanya kazi kwa moyo sana ila hakuweza kuendelea kuwa na moyo huo huo. Alichoka sana na siku zilivyozidi kwenda alikata tamaa na hakuona tena nafasi ya kununua uhuru wake.
Aliendelea kujipa moyo na kufanya kazi na siku moja alikuja kuchukuliwa na kurudishwa babeli. Alifukua mfuko wake wa fedha na kuondoka. Alipofika babeli alishangaa kuona anapelkwa kwa yule rafiki yake ambaye ni babu wa huyo kijana aliyekuwa akimhamasisha. Alimwambia kwamba amemtafuta kwa muda mrefu mpaka aliposikia kwamba alichukuliwa na mtu mwingine na hivyo ikabidi amnunue kama mtumwa. Alimwambia wanaelekea Damascus na anamhitaji yeye awe mshirika wake kwenye biashara kwa sababu amependezwa na moyo wake wa kupenda kufanya kazi kwa bidii. Sharru alitokwa na machozi na alijiona kama mtu mwenye bahati sana na pia aliendelea kuamini na kukubali kwamba kazi haimtupi mtu. Ni utayari wake wa kufanya kazi uliomfanya aweze kukutana na mtu yule muhimu kwenye maisha yake.
Alimwambia kijana yule wkamba babu yake alipenda kazi na hivyo kazi iliweza kumlipa vizuri, Na pia alimwambia kwamba kazi ni kwa kila mtu na sio kwa watumwa tu kama alivyokuwa anafikiri yeye. Kijana yule alimsukuru sana Sharru Nada kwa historia ile na alimwahidi kwamba atakuwa kama alivyokuwa babu yake. Atafanya kazi kwa juhudi sana ili aweze kufikia mafanikio kama aliyofikia babu yake.
Umejifunza nini kwenye hadithi hii ya Sharru Nada?
Kuna mambo zaidi ya kumi tunayoweza kujifunza kupitia hadithi hii, hasa ukilinganisha utumwa wa sasa ambao ni ajira na jinsi watu wengi wanavyoshindwa kufikia mafanikio. Tushirikishe kwenye maoni hapo chini mambo matano uliyojifunza katika hadithi hii.
Nakusihi uandike mambo hayo matano hapo chini maana itakuongezea wewe kuelewa zaidi na kuweza kuchukua hatua. Fanya hivyo na yafanyie kazi yale uliyojifunza.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kufikia mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.
Kwenye simulizi hii nimejifunza mengi. Baadhi ni 1. Kazi haimtupi mtu: Jitume kufanya kazi kwa moyo mmoja,kwa bidii na maarifa hata kama ni kazi ngumu na ya unyanyasaji na mateso,hata kama hakuna anayekuona na kukushukru ama kukupa pole fanya kazi kwa wema na mwisho wa yote utapata fadhila na maisha yatanyooka. 2.kila mtu ni mtumw. Eidha wewe ni mtumwa wa binadam mwingine ama mtumwa wa tabia zako mbaya,walioko huru ni wale walioelewa utumwa wao na kuchukua hatua za kuondoka kwenye utumwa huo. Hivyo tunahitaji kujiuliza sisi ni watumwa wa nani? Au Wa kitu gani? Na tuchukue hatua za kudai uhuru wetu. 3.Ni muhimu kufanya kazi kwa bidii na maarifa bila ya kujali kiwango cha ko cha mafanikio.Eidha we ndo unafanya kazi ama unao wafanyakazi hivyo wewe ni bosi fanya kazi kwa bidii na maarifa ili kufikia mafanikio makubwa zaidi. 4. Kuwa na fedha nyingi kunakupatia uhuru wako uliopoteza.Hivyo kila mtu anayetaka kuwa huru na maisha yake hana budi kupata maarifa(taarifa)sahihi juu ya fedha. 5.Ni muhimu kujua kuuza unachouza ili kufikia mafanikio makubwa mfano:Sharru alijua kuuza upishi wake na akakubalika kwa bwana wake na pia alijua kuuza keki zake na akakubalika kwa wateja wake.
LikeLike
Asante sana Ngutiti kwa kutushirikisha haya uliyojifunza.
Tuyafanyie kazi ili tuweze kubadili na kuboresha maisha yetu.
LikeLike
Nimejifunza mambo mengi ila la kwanza kabisa
1.kupenda kile unachokifanya kama hyu bwana alipenda kujifunza kupika keki na akapika kwa kupenda mwenyewe bila kulazimishwa na ndio maana zikawa nzuri. 2.kazi zote ni utumwa ili uondokane na utumwa lazima ufanye kazi sana ili upate mafanikio makubwa uwe huru.3.kuwa na marafiki wanaotia moyo sio wanaokukatisha tamaa.
4.kuwa na watu unaotamani kuwa kama wao.
5. Juhudi zozote huwa lazima zizae matunda.
LikeLike
Asante sana kwa kutushirikisha uliyojifunza.
Sasa yafanyie kazi ili kuweza kuboresha zaidi maiosha yako.
TUPO PAMOJA.
LikeLike
Sharru amenifunza bidii ameonekana mwenye bidii Sana na kujali anachofanya anapenda kujifunza pia anaweka Akiba Licha ya hekaheka Zote za utumwani lakini alikumbuka kuweka Akiba
LikeLike
Hakika,
Na hili ndiyo kila mmoja wetu anapaswa kufanya pale anapopitia changamoto kwenye maisha yake.
LikeLike
1-Kufanya kazi kwa bidii bila ukataa taamaa
2-kupenda sana kazi yako
3-kuwa mvumilivu
4-kupenda kujifunza kwa biiidi
5- kuweka fedha kwa bidii
LikeLike
Vizuri sana Jedo.
LikeLike
Katika hadithi hii nimejifunza mengi sana, baadhi ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa; kutokuta tamaa, kujifunza kila siku kuhusu kazi unayofanya au unayotaka kufanya; kuwa na maono na malengo ya muda mrefu; kuepuka njia za mkato katika kutafuta mafanikio, Sifa ya mshirika bora wa kushirikiana naye biashara; kuwa na uvumilivu pale mambo yanapokwenda tafauti, Huwezi kuwa huru kama huna fedha yako mwenyewe; utumwa sio ajira pekee hata tabia zako mwenyewe zinaweza kukufanya kuwa mtumwa. Kuondoka kwenye utumwa ni kufanya kazi kwa bidii kwani kazi haimtupi mtu.
LikeLike