anawauliza wananchi, wangapi wanataka mabadiliko? Wote wananyoosha mikoni.
Anauliza swali la pili wangapi wanataka kubadilika? Hakuna hata mmoja ananyoosha
mkono.
Hivi ndivyo maisha ya watu wengi yalivyo, kila mtu anataka
mabadiliko, anataka maisha yake yawe bora, anataka kuwa na kazi au biashara
nzuri, anataka kuwa na familia bora, anataka kuwa na uongozi mzuri na mengine
mengi mazuri. Lakini inapokuja swala kwamba inabidi mtu abadilike hapo ndio
changamoto inapoanza.
SOMA; MUDA–Kitu Chenye Thamani Kubwa Ila Kisichothaminika Na
Wengi.
Hakuna ambaye anataka kubadilika, japo kila mtu anataka
mabadiliko. Kila mtu anataka aendelee kufanya kile ambacho amezoea kufanya,
anataka kuendele ana masiah ambayo ameyazoea, lakini anataka kuona mabadiliko
makubwa. Hii ni ndoto ya mchana ambayo haiwezi kutokea kwa njia yoyote
ile.
Mabadiliko yanaanza na wewe na ndio vitu vingine vinabadilika.
Unabadilika kwanza wewe na ndio kazi yako, biashara yako, mwenza wako, watoto
wako, wafanyakazi wako na jamii inayokuzunguka wanabadilika. Haiendi kinyume na
hapo, kwamba hivyo vingine vyote vikishabadilika basi na wewe ndio utabadilika,
usipoteze muda wako, hakuna kitu kama hiko.
Unataka kufikia mafanikio makubwa kwneye maisha yako? Haya hapa
ni mabadiliko kumi unayotakiwa kuyafanya sasa, yaani leo hii hii kama bado
umekuwa huyafanyi.
1. Kuwa na matumizi mazuri ya muda wako, usiupoteze kwa mambo
yasiyokuw aya msingi kwako.
2. Usishiriki kwenye majungu, umbeya au kumsema mtu
vibaya.
3. Weka juhudi kubwa sana kwenye kazi yako, nenda hatua ya
ziada, fanya zaidi ya mtu mwingine yeyote.
4. Acha matumizi mabovu ya fedha, nunua vitu ambavyo ni muhimu
kwako.
5. Acha kukaa na watu ambao wanakurudisha nyuma.
SOMA; Mitandao Ya Kijamii, Kazi na Mapumziko.
6. Pata muda wa kukaa na familia yako na wale
unaowapenda.
7. Usinunue kitu ili kuonekana, au kwenda na wakati.
8. Kuwa mwaminifu, kuwa mwadilifu.
9. Timiza neno unaloahidi.
10. Sema hapana mara nyingi uwezavyo. Jambo lolote ambalo halina
manufaa kwako au halitakufikisha kwneye malengo yako sema hapana.
Anza na hayo machache, halafu niandikie yale mabadiliko
utakayokuwa unayaona kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TAMKO LA LEO;
Najua hakuna mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kutokea nje
yangu. Mabadiliko yoyote ya kweli yanaanza na mimi. Kama kuna kitu chochote
nataka kibadilike kwneye maisha yangu, mimi ndio wa kwanza
kubadilika.
Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza
hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.