Makirita kuna tatizo gani tena? Mbona mimi sijajiua? Sawa sawa, hujajiua, ila subiri kidogo tuone kama utetezi wako ni wa kweli au la.

PAAAAA, HALAFU TUNASAHAU KUHUSU WEWE....
PAAAAA, HALAFU TUNASAHAU KUHUSU WEWE….

Kabla hatujaendelea kwanza ulishasoma makala HIVI NDIVYO UNAVYOKUFA NA MIAKA 35 NA KUZIKWA NA MIAKA 65? Kama bado bonyeza hayo maandishi uisome. Halafu kuna nyingine tena inaitwa HIKI NDIO KITAKACHOTOKEA MIAKA 100 IJAYO, hata kama ulishaisoma, tafadhali isome tena, bonyeza hayo maandishi kuisoma. Kumbuka kurudi hapa baada ya kuzisoma, na usiendelee kusoma kabla hujasoma makala hizo mbili.

………………….

Karibu tena, naamini umeshasoma makala hizo mbili. Kama bado rudi kazisome, usiwe na haraka, utaelewa vizuri zaidi kile tutakachojadili leo kama utakuwa na msingi wa makala hizo mbili.

Sasa nataka nikuambie kwa nini unajiua kabla hata ya muda wako.

Kwanza kabisa ukishakufa hakuna unachoweza kubadili tena kwenye maisha yako. Unafikiria kumpigia simu mzazi wako lakini unasahau, ukishakufa leo hutaweza kupiga tena hiyo simu. Si ndio?

Sasa kwa nini umekuwa unaishi maisha kama vile tayari umeshakufa? Maisha ambayo hayabadiliki? Maisha ambayo yanafanana na ya kila mtu kama vile ambavyo maisha yetu yatabaki kufanana tukishakufa?

Unalalamika kwamba kazi unayofanya huipendi, haikupi kipato na huoni kama unatoa mchango wako kupitia kazi hiyo. Sasa kwa nini usibadilishe? Hujafa, unaweza kufanya chochote unachotaka na maisha yako. Ukifa leo historia itakayosomwa na itakayobakia ni kwamba ulifanya kazi hiyo, ambayo huipendi hata chembe kutoka moyoni mwako.

Kwa nini usianze kufanya mabadiliko sasa kwenye maisha yako? Muda unao, uwezo unao, unasubiri nini? Au unajidanganya kwamba muda bado upo? Kumbuka hata anayevuta pumzi yake ya mwisho wakati unasoma hapa, alifikiri anao muda wa kutosha. Ndio kawaida yetu binadamu, hivyo unahitaji maamuzi dhabiti kuondokana na hilo.

Tafadhali sana usijiue kabla muda wako haujafika, kitu chochote hukipendi kwenye maisha yako unaweza kukibadili sasa hivi. Usisubiri zaidi, maana huna muda wa kutosha kama unavyofikiri.

TAMKO LA LEO;

Nimegundua kwamba nimekuwa najiua mwenyewe kabla hata ya muda wangu. Nimekuwa naishi maisha ambayo hayabadiliki licha ya kuwa na nafasi nyingi za kuyabadili. Nimekuwa naona kama nina muda mwingi w akufanya jambo lolote ninalotaka kufanya kumbe nimekuwa najidanganya. Naanza kuishi sasa, sio kesho wala siku zijazo. Naanza kuishi sasa na chochote ambacho sipendi kwenye maisha yangu naanza kukibadili sasa hivi. NDIO SASA HIVI.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.