Akili Ni Nywele Kila Mtu Ana Zake, Je Unamjua Adui Wa Akili Yako?

Mara nyingi tunasikia msemo huu akili ni nywele kila mtu ana zake, lakini umeshawahi kujiuliza ni nani ambaye ni adui wa akili yako ?

UMESHAMJUA ADUI YAKO?

 
Mkurugenzi wa kampuni ya Amka Consultants, katika kurasa 365 alizojiwekea, yaani utaratibu wake wa kuandika kila siku ukurasa mmoja kwa mwaka ni jumla ya kurasa 365, katika ukurasa wake wa 201 aliandika hivi ‘’ kama unataka kufanikiwa achana na demokrasia na kuwa dikteta’’ (kusoma ukurasa huo bonyeza maandishi haya) katika ukurasa huo wa 201 anaeleza kuwa ukiipa akili yako demokrasia hutofika mbali na ukiendekeza kuisikiliza akili yako hutofanikiwa, mfano umepanga kuamka mapema akili yako inakukataza usiamke sasa ukishaipa nafasi tu umekwisha baadaye unaanza kulalamika laiti ningelijua lakini kama ungekuwa dikteta usingeipa nafasi ungeamka mapema na kutekeleza wajibu wako. Mpaka hapa umeshaanza kujua nani adui wa akili yako. Hivyo basi unahitaji kuwa dikteta wa akili yako ndio utaweza kufanya jambo kubwa kwenye maisha yako.
Sasa turudi katika mada yetu ya leo tumjue nani adui wa akili yako, adui wa akili yako ni kama ifuatavyo endelea kusoma utamjua adui wa akili yako;
i) Adui namba moja wa Akili yako ni WEWE MWENYEWE
Ukatae au ukubali ila adui namba moja wa akili yako ni wewe mwenyewe. Wewe ndio unaidumaza akili yako akili yako inaweza kukupa mawazo mazuri ya kufanya jambo fulani ambalo litakuletea mabadiliko chanya juu ya maisha yako. Lakini wewe unaidhulumu akili yako unakuwa adui hutaki kuthubutu kutokana na wazo zuri la kufanya jambo fulani ambalo ulipata kutoka katika akili yako. Unaendelea kulalamika bila kuchukua hatua. Kulalamika bila kuchukua hatua ni kudumaza akili yako.
Akili yako inahitaji maarifa chanya kila siku ili iweze kukua, Je unalisha ubongo wako kila siku? Unalalamika huna muda wa kusoma vitabu, makala nzuri lakini muda wa kufuatilia vitu hasi ambavyo havikuingizii chochote. Natumaini mpaka hapa umeshamjua adui wa akili yako? La hasha! Jibu ni wewe mwenyewe ambaye unasababisha yote haya. Akili yako ni kiwanda kinachozalisha mawazo mazuri, hivyo tumia vema akili yako.
Unaweza kuidumaza akili yako wewe mwenyewe kupitia mambo haya;
Kupitia usingizi, kwa binadamu anatakiwa kulala masaa 8-9 kama wanavyotushauri wataalamu wa afya. Lakini kuna watu wengine wanaharibu mambo yao mengi kwa kuendekeza usingizi, wanalala zaidi ya masaa elekezi ya wataalamu wa afya. Unaamka ukiwa umechoka, unaanza siku yako kwa kusikiliza habari badala ya kuanza kuingiza maarifa katika akili yako kwa kusoma kitabu. je kwa kufanya siyo kuwa adui wa akili yako?
Kupitia kuahirisha mambo, katika maisha ya kila siku tumetawaliwa sana na kuahirisha mambo, umepanga kufanya kitu kizuri umepata mawazo mazuri kutoka katika ubongo wako lakini hutaki kuthubutu unaahirisha jambo hilo kwa kufanya hivyo unakuwa adui wa akili yako.
Kupitia kukata tamaa, kukata tama ni dhambi kubwa katika maisha ya mtafutaji, unapokata tamaa katika jambo lolote lile unakuwa adui wa akili yako unaipa woga akili yako unaifanya iwe dhaifu na kukupa mawazo ya kushindwa tu na siyo kushinda.
SOMA; Mambo 5 Ambayo Yanaweza kufanya Maisha Yako Kuwa Mafupi.
ii) Woga
Sisi sote tulizaliwa bila woga. Mtoto mdogo anapozaliwa anakua hana woga kumbe sisi sote tulizaliwa bila woga na tunajifunza woga kupitia maisha yetu ya kila siku. Moja ya vitu ambavyo ni adui wa akili yako ni woga, unataka kufanya jambo zuri lakini unashindwa kwa sababu ya woga kwa hiyo kwa kufanya hivi unakuwa adui wa akili yako.
iii) Wasiwasi
Una jambo zuri la kufanya au kusema unashindwa kwa sababu ya wasiwasi na wasiwasi unasababishwa na kutojiamini, kama huamini mawazo yako basi huamini akili yako. Kwa hiyo wasiwasi ni moja ya adui wa akili yako, kataa leo hali ya kuwa na wasiwasi, jifunze ili uweze kuwa imara katika kile unachofanya utaondoa wasiwasi na mashaka katika maisha yako amini unaweza na utaweza kweli lakini ukiendelea na hali ya mashaka tu unakuwa adui wa akili yako.
Kwa hiyo tumeona kuwa adui wa akili yako ni wewe mwenyewe. Nakutakia mabadiliko chanya katika akili yako kwa sababu umeshamfahamu adui wa akili yako.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: