Kila siku mpya ni mbegu mpya ambayo kama ukiweza kuipanda vizuri utakuwa na mavuno mazuri sana baadae.
Usikubali siku yako iishe kama vile ambavyo wengine wanafanya.
Wewe ichukulie siku yako kuwa ya kipekee,
Ione kama nafasi ya kuionesha dunia ubora ambao uko ndani yako, ubora ambao dunia haijawahi kuuona.
Na hilo unaanzia kwa kile ambacho unakifanya, nenda hatua ya ziada, ongeza thamani.
Wewe kama mwanamafanikio usikubali kabisa kufanya kwa mazoea, maana kufanya hivyo ni kuamua kuipoteza siku yako.
Weka kitu cha tofauti, ongeza ubora, ongeza thamani.
Dunia inalipa zaidi kwa thamani kubwa. Sasa kwa nini wewe ukose nafasi hii?
Anza sasa.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani.
Siku Mpya Ni Mbegu Mpya, Unaipanda Wapi?
