Kuna njia kuu mbili za kushinda, njia zote ni muhimu sana kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa. Lakini cha kushangaza watu wengi wanajua njia moja pekee. Njia ya pili hawaijui, japo ndio njia muhimu kuliko ile inayojulikana na wengi.

KUSHINDA NA KUSHINDWA NI NJIA MBILI ZINAZOKUPELEKA SEHEMU MUJA, MAFANIKIO.
KUSHINDA NA KUSHINDWA NI NJIA MBILI ZINAZOKUPELEKA SEHEMU MUJA, MAFANIKIO.

Njia ya kwanza ya kushinda ni kushinda. Ndio, ulipanga kufanya kitu fulani na umekifanya, basi wewe ni mshindi. Bi njia inayokupeleka kwenye mafanikio kwa kuweza kufanya kile ambacho umepanga kufanya.

Njia ya pili ya kushinda ni kushindwa. Ndio, ulipanga kufanya kitu fulani lakini umeshindwa kukifanya. Hapa unaweza kuona wewe ni mshindwa, lakini kiuhalisia wewe ni mshindi kwa sababu sasa unajua njia ambayo haiwezi kuleta majibu unayotaka. Unakuwa umeshinda kwa sababu tayari unajua njia ambazo hazitaleta majibu mazuri.

Njia hii ya pili ni muhimu sana kwa sababu itakuokolea muda mwingi sana. Watu wengi huwa hawalioni hili na hivyo kupoteza nafasi nzuri ya kujifunza kutokana na kile ambacho umeshindwa kufanya.

Kama utakuwa hujui njia ya pili ya kushinda ambayo ni kushindwa, hutaweza kuitumia vizuri kwa ajili ya mafanikio.

TAMKO LA LEO;

Sasa nimejua mafanikio hayatokani na kushinda tu, bali hata kushindwa pia. Kuna mambo mengi sana ninayoweza kujifunza pale ninaposhindwa kufanya kitu na kama nikiyatumia nitajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kushinda baadae. Nakubali kwamba kuna njia mbili za kushinda na kufika kwenye mafanikio makubwa. Njia ya kwanza ni kushinda na njia ya pili ni kushindwa. Kwa njia zote hizo mbili nakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua ni njia ipi itanifikisha kwenye mafanikio na ipi haitanifikisha.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.