Baada ya kufanya kazi iliyo bora sana kwa uwezo ulionao.

Baada ya kutoa huduma iliyo bora sana kwa wateja wako.

KILA SIKU WEKA UBORA ZAIDI YA SIKU ILIYOPITA, HIVI NDIVYO MAFANIKIO MAKUBWA YANAVYOFIKIWA.
KILA SIKU WEKA UBORA ZAIDI YA SIKU ILIYOPITA, HIVI NDIVYO MAFANIKIO MAKUBWA YANAVYOFIKIWA.

Baada ya kuandika makala/kitabu kilicho bora sana kwa uwezo wako.

Baada ya kuweka kila ulichonacho kwenye kitu ambacho unafanya.

Na bado watu wasione kama umefanya kitu kikubwa.

Unahitaji kuendelea kufanya tena na tena na tena.

Kwa sababu mafanikio hayatokani na kufanya kilicho bora mara moja, bali kufanya kile kilicho bora mara kwa mara mpaka inakuwa ndio kawaida yako.

Kufanya mara moja na kuacha kwa sababu hukupata ulichotarajia, ni kupoteza muda wako.

Na hata kama ulifanya kazi iliyo bora na kupata mafanikio makubwa, usijisahau na kuona ndio umefika kileleni, endelea kuweka ubora zaidi kila siku.

Maana utakapojiona kwamba ndio umefika kileleni ndio mwanzo wa kuporomoka.

TAMKO LA LEO;

Najua mafanikio hayatokani na mimi kufanya kilicho bora kwa mara moja tu. Bali mafanikio yanatokana na mimi kufanya kilicho bora kila mara. Nimeshaamua kwamba chochote nitakachofanya, ni lazima nikifanye kwa ubora wa hali ya juu sana kwa sababu nimechagua maisha ya mafanikio. Na hata nitakapofanya kazi ya ubora wa hali ya juu, sitaishia pale, bali nitaendelea kuongeza ubora zaidi kila siku.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.