Sababu kubwa sana inayowafanya watu wengi kukata tamaa ni pale wanapofikiri kwamba ni wao. Pale ambapo wanaambiwa hapana, moja kwa moja wanachukulia kwamba hapana ilikuwa ni kwao.

Unaanzisha biashara na kuna mtu ambaye ulijua kabisa angekuwa mteja wa biashara yako, lakini unapomwambia anakuambia hapana. Na wewe unachukulia kwamba hapana ile ni kwako wewe, umekataliwa. Lakini ukweli ni kwamba hapana hii sio kwako wewe bali ni kwa biashara yako.

HAKUNA MTU ANAYEKUKATAA WEWE, BALI WANAKATAA KILE UNACHOTOA, KIBORESHE.
HAKUNA MTU ANAYEKUKATAA WEWE, BALI WANAKATAA KILE UNACHOTOA, KIBORESHE.

Unatoa mawazo mazuri kwenye eneo lako la kazi, au hata kwenye familia na watu wanasema hapana. Moja kwa moja unachukulia kwamba wewe umekataliwa. Lakini sio wewe uliyekataliwa, ni mawazo yako uliyonayo sasa ndio yamekataliwa.

SOMA; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.

Unapoambiwa hapana kwenye jambo lolote, hapana ile sio kwako wewe binafsi, bali ni kwa kile unachofanya au kusema. Ukilijua hili na kulifanyia kazi utaona fursa nyingi na nzuri. Lakini kama utachukulia hapana hizi ni kwako binafsi takata tamaa na kuacha kabisa kufanya kile ulichokuwa unafanya.

Ila unapojua kwamba hapana sio kwako wewe binafsi, unaboresha zaidi kile ambacho kimekataliwa na siku moja kila mtu atasema ndiyo.

Hapana yoyote utakayoambiwa kuanzia leo, usiichukulie binafsi, chukulia ni kile unachofanya bado sio bora na endelea kuboresha. Hakuna mtu anayekuchukia wewe ila kila mtu anapenda kitu kilicho bora. Wekeza kwenye kutoa kilicho bora zaidi na kila mtu atasema ndiyo.

TAMKO LA LEO;

Nimejua ya kwamba mtu anaponiambia hapana kwenye kitu ninachofanya au kusema hasemi hapana kwangu mimi binafsi, bali anasema hapana kwa kitu kile. Kuanzia sasa nitaacha kuzichukulia hapana kama kitu binafsi na badala yake nitazitumia kuboresha zaidi kile ninachotoa kwa wengine. Hii itanisukuma kusonga mbele zaidi badala ya kukata tamaa.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.