Ni rahisi sana kulaumu wengine pale mambo yanapokwenda vibaya.
Ni rahisi sana kulalamikia chochote unachoweza pale unaposhindwa kufikia ulichotaka kufikia.
Lakini mara nyingi na kwa sehemu kubwa sana ni wewe uliyesababisha kufika hapo ulipofika sasa.

Ni wewe uliyeamua kula vyakula vya hovyo na sasa afya yako inasumbua.
Ni wewe uliyekubali kuingia kwenye kazi hiyo na sasa inakutesa.
Ni wewe uliyesema ndio kwa mahusiano hayo ambayo yanafanya maisha yako kuwa magumu.
Ni wewe uliyeamua kutumia kila unachopata bila ya kuweka chochote pembeni, na sasa unashangaa japo umefanya kazi miaka mingi huna cha kujivunia.
Ni wewe uliyeamua kuwaamini watu hao ambao sasa wamekutapeli au wamekuingiza kwenye matatizo.
Ni wewe uliyeamua kutokuwekeza kwenye mahusiano yako, na sasa yameingia kwenye matatizo makubwa.
SOMA; Ukiwa Unakula Chakula Kitamu, Hujali Serikali Inafanya Nini.
Kila kitu kinachotokea kwenye maisha yako leo, ulikitengeneza wewe mwenyewe siku zilizopita. Hivyo badala ya kuangalia ni nani wa kumlaumu au kipi cha kulalamikia, angalia kwanza ni mchango gani umekuwa nao kwenye eneo hilo na chukua hatua.
Kulalamika na kulaumu ni rahisi, lakini hakutatui tatizo. Sasa wewe unataka nini? Kuboresha maisha yako au kuendelea kuwa na maisha yako? Kama ni kuboresha acha kulalamika na chukua hatua. Kama unataka yaendelee kuwa hovyo endelea kulalamika na kutafuta wa kulaumu.
TAMKO LA LEO;
Najua chochote ambacho kinatokea kwenye maisha yangu kwa sasa nimekitengeneza mimi mwenyewe kwa siku za nyuma. Najua ni rahisi sana kulalamika na kulaumu, ila hayo hayatatui tatizo la msingi ninalopitia sasa. Sitapoteza muda wangu kulalamika au kulaumu, nitaangalia ni hatua gani ninaweza kuchukua na nitaichukua mara moja.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.