Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu The Life-Changing Magic Of Tidying Up (Maajabu Ya Kupangilia Vitu Vyako Vizuri).

Habari ndugu msomaji wa makala za uchambuzi wa vitabu. Hii ni wiki nyingine, ninamshukuru Mungu kwa ajili yako kwa uzima na afya tele aliyokujalia. Nipende kukukaribisha katika makala za mambo 20 kutoka kwa kitabu. Wiki hii kitabu chetu kinaitwa The life Changing magic of tidying up. Kitabu hiki kimeandikwa na mwana mama wa Kijapan anaitwa Marie Kondo. 
Mwandishi anaelezea maajabu yapatikanayo katika kupangilia vizuri vitu katika nyumba tunazoishi au maofisini, mkazo mkubwa umekua ni jinsi ya kuboresha mazingira ya nyumbani. Mwandishi anaelezea kwamba mtu anaweza kubadili maisha yake kwa kupangilia vizuri nyumba yake. Pia kutokana na utamaduni wa kijapan ni kwamba usafi wa nyumba unavutia bahati na baraka. 

Kitabu hiki pia kinafundisha jinsi unavyoweza kupata furaha kwa kuondokana na msongamano wa vitu vingi visivyokua na faida kwako, na kubakia na vitu vichache vile vyenye umuhimu tu unavyoweza kuvifurahia ukiwa navyo. Kitabu hiki kinafunza mambo mengi sana, haya mambo 20 ni machache sana ukilinganisha na yaliyomo kwenye kitabu.
Karibu tujifunze
1. Nyumba au chumba ambacho hakijapangiliwa kinatoa taswira ya jinsi gani kichwani pako pia ambavyo hakujapangiliwa. Kua na mpangilio mzuri ni swala la mindset, linaanzia kwenye akili yako. Kama unaweza kuishi mahali ambako pako rafu, na wala usione tatizo, basi unapaswa kufahamu kua tatizo liko kwenye akili.
2. Upangiliaji wenye ufanisi unahusisha matendo mawili muhimu: (1) Kuondokana/kuondoa (2) kuamua wapi pa kuhifadhi vitu. Kanuni hii haibadiliki.
3. Anza kwa kuondokana au kutupilia mbali (discarding) kwanza mpaka umalize ndipo uende kwenye kuhifadhi na kupangilia. Mfano kwenye kutengeneza mpangilio mzuri wa nguo zako, anza kwanza kwa kuondoa zile ambazo huzihitaji, kama zile ambazo hazikutoshi na zile ambazo huzivai kwa muda mrefu. Ondoa na weka kando, kisha zibaki zile tu unazozihitaji. Hapo sasa ndio uende hatua nyingine ya kuhifadhi. Start by discarding, all at once, intensely and completely
4. Kabla hujaanza zoezi la kuweka mpangilio kwenye nyumba au ofisi yako, kwanza pata taswira ya hatima unayotaka kuifikia. Yaani pata picha unataka uwe na mpangilio wa aina gani na wa kiwango gani. Kwa maneno mengine baada ya kupangilia na kusafisha nyumba yako unataka ionekane namna gani. Ukishapata picha ya mwisho jinsi unataka nyumba au ofisi yako ionekane, itakupa hamasa ya kuanza mchakato. Before you start, visualize your destination
5. Fanya upangiliaji kwa makundi na sio kwa eneo (tidy by category not by Location). Mfano unayo vyumba viwili na kila chumba kina nguo, kuna nyaraka (documents), kuna viatu, vitabu n.k Ukipangilia kwa maeneo itakua unarudia rudia kitu ambacho kitakufanya ushindwe kumaliza. Yaani ukifanya kwa kuzingatia maeneo (Vyumba) utajikuta kila chumba unarudia kupanga nguo, kupanga vitabu, kupanga nyaraka n.k. Hivyo zoezi kuonekana refu na gumu. Lakini ukifanya kwa kuzingatia makundi ya vitu, mfano ukaanza na nguo. Unakusanya nguo zote mahali pamoja (kutoka vyumba vyote), kisha unaanza zoezi. Ukimaliza nguo unahamia kundi lingine kama la vitabu, kisha unaendelea mpaka umalize makundi yote.
SOMA; USHAURI; Umekuwa Kwenye Kazi Muda Mrefu Na Huoni Mafanikio? Zingatia Mambo Haya Muhimu Sana.
6. Anza na vile vitu ambavyo ni rahisi kwako kufanya maamuzi. Katika kuondoa au kutupa vitu, akili inafanya kazi ya kufanya maamuzi kama hichi unakihitaji au haukihitaji. Vile usivyovihitaji ndivyo unavyotakiwa kuondokana navyo au kwa lugha nyepesi kuvitupa. Sasa katika zoezi hili la kutupa vitu, anza na kundi la vitu ambavyo ni rahisi kufanya maamuzi. Mfano ukianza na picha, itakuwia vigumu, maana maamuzi ya picha zipi za kutupa, hutayafanya kirahisi. Lakini kama ni nguo, unajua hii hua haikutoshi, unaweka kando, unajua hii hua nikivaa sipendezi nayo unaweka kando. Mpaka ubakie na zile unazohitaji tu. Jambo la kuzingatia hapa ni kuanza na makundi ya vitu ambayo itakuwia rahisi kufanya maamuzi, kipi cha kuondoka na kipi cha kubaki. The process of deciding what to keep and what to discard will go much more smoothly if you begin with items that are easier to make decisions about.
7. Katika kuchagua kipi cha kuondoa kipi cha kubakiza, hakikisha unabakiza vichache tu vile ambavyo unahisi ukibaki navyo utavifurahia. Haina maana kubaki na vitu kibao ambavyo hata hukumbuki kama unavyo. Mfano yafaa nini kua na nguo ambazo una miezi minne au mwaka hujawahi kuzivaa? Bakiza chache ambazo una matumizi nazo.
8. Wagawie wengine vile vitu ambavyo huna matumizi navyo. Ukimaliza zoezi la kuweka pembeni vile usivyovihitaji. Angalia ni vipi katika hivyo vitahitajika na mwingine. Ila hakikisha kwamba kweli huyo unayempa anavihitaji, isije kua na yeye anakwenda kuviweka tu, likawa na kwake tatizo la kurundika vitu. Ikiwezekana unaweza kuuza hata kwa bei ndogo, ambapo mtu atanunua kama kweli anauhitaji nacho. Giving things you can’t use to others who can is an excellent idea.
9. Katika maisha Sio kila mtu ambaye unakutana naye katika maisha atakua rafiki yako au mpenzi wako. Kuna ambao itakua ngumu kwako kuwapenda, au kuambatana nao. Lakini watu hao pia wanatupa funzo la ku appreciate wale ambao ni wa muhimu. Vivyo hivyo basi hata katika vitu unavyokutana navyo si vyote vitakua vya muhimu kwako, lazima uwe na mtazamo huu, ili isikuwie vigumu kuondokana navyo.
10. Ili uweze kufurahia vitu ambavyo ni muhimu kwako, lazima kwanza uondokane na vile visivyo vya muhimu. Vile vilivyo kwisha kumaliza kusudi lake vinapaswa viondoke, ili uone umuhimu wa vitu vipya.
SOMA; KITABU CHA SEPTEMBA; Guide To Investing(Muongozo Wa Uwekezaji).
11. Vile unavyovaa ukiwa nyumbani vina athari katika taswira yako. Kuna watu wakiwa nje na nyumbani wanakua nadhifu (smart) ila wakiwa nyumbani wanavaa hovyo/rafu. Kile unachojifanyia au kufanya pindi ukiwa peke yako kina athari sana kwako kuliko kile unachofanya ukiwa mbele za watu. Maana unapokua mwenyewe ndipo uhalisi wako unajidhihirisha. Hivyo basi vile unavyovaa ukiwa nyumbani ndivyo vinavyoakisi taswira yako zaidi. Sasa yakupasa kuanza kuvaa vizuri hata unapokua mwenyewe nyumbani, maana kwanza hii ni njia ya kuonyesha unajipenda, bila kujali nani yupo nani hayupo. What you wear in the house does impact your self-image.
12. Katika kuhifadhi nguo kuna njia mbili: ya kwanza ni ile ya kuzining’iniza kwa kutumia vifaa vya kutundikia au unaweza kuziita Hangers. Njia ya pili ni ile ya kukunja nguo na kuziweka kabatini au mahali pengine. Ila wengi wanapenda kutumia hiyo ya kwanza ya kutundika maana inaonekana ndio rahisi. Japo njia inayopendekezwa ni hiyo ya pili ya kuzikunja. By neatly folding your clothes, you can solve almost every problem related to storage.
13. Katika upangiliaji wa vitabu. Kwanza weka vitabu vyote chini sehemu moja. Anza kwa hatua ya kwanza ya kutenga vile visivyohitajika. Kisha ukimaliza vile vinavyotakiwa kubaki, ndio uanze kuvipanga katika makundi mbali mbali: Mfano vitabu vya ujumla (general), vitabu vya biashara, vitabu mahusiano. N.k
14. Katika kuamua kitabu kipi kiondoke na kipi kibaki, kigezo kiwe ni kama unapata furaha au la pindi unapokishika. Kumbuka ni kwa kukishika tu, na sio kukisoma. Maana ukishafungua na kujaribu kupima kwa kusoma, basi zoezi litakushinda, maana utajikuta karibu vyote unavibakiza, na kubaki na mrundikano wa vitabu ambavyo wala hutaweza kuvisoma.
15. Kufahamu hasa unahitaji kitu gani. Lazima kwanza uondokane na vile visivyokua vya muhimu kwanza. Huwezi kufahamu unahitaji nini kama umezongwa na vitu kibao ambayo wala havina mchango wowote kwako. Lazima uanze kuvitupa kando nipo sasa akili yako inaweza kufikiria na kutambua ni kitu gani unakihitaji. The best way to find out what we really need is to get rid of what we don’t.
SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha How To Live On 24 Hours A Day.
16. Chumba au nyumba iliyopangiliwa vizuri, inafanya akili nayo inakua imetulia, na utakua unavutiwa mara kwa mara kukaa nyumbani kwako. Ukiwa na sehemu nzuri iliyopangwa vizuri akili yako itaanza kugundua kusudi/wito wako. Upo ushahidi kwa watu wenye kuwaza mawazo makubwa ya kibiashara, pindi walipoweza kubadilisha maeneo wanayokaa kwa kuyafanya kua na mpangilio mzuri.
17. Katika kuhifadhi na kupangilia vitu: Kwa kundi la vitu au kwa makundi ya watu. Kama unaishi kwenye familia ya watu kadhaa, kitu cha kwanza ni kutengeneza sehemu ya kuhifadhi ya kila mwanafamilia. Kwa mfano kama ni nguo na familia ina Baba, mama, John na Joyce. Kila mmoja anakua na sehemu yake ya kuhifadhia nguo, na sio nguo zao wote kuweka sehemu moja. Kadhalika na kwa vitu vingine.
18. Ukishaweka mpangilio wa vitu vizuri, kila kitu kikaa sehemu yake. Kinachobakia ni zoezi la kurudisha kitu mahali pake. Mfano kama ni kitabu, umechukua kwenye eneo ulilolitenga kwa ajili ya vitabu, ukimaliza ina maana inapaswa kurejesha pale ulipotoa. Ukiona nyumba uliyoipangilia awali, baada ya muda imeanza kupata msongamano wa vitu, basi ujue tatizo hapo ni kushindwa kurudisha vitu mahali pake panapohusika. Hii ina maana kwamba pamoja na kuweza kupangilia vizuri nyumba yako lazima uwe na nidhamu ya kurudisha vitu mahali pake husika.
19. Katika kuhifadhi vitu usipange kwa kupandiana (Never pile things), Badala yake vipange kwa wima (Vertical storage). Mfano kama ni vitabu usipange kitabu juu ya kitabu, badala yake unavipanga kwa wima. Hata nguo zikikunjwa vizuri zinapangika kwa wima. When it comes to storage, vertical is best.
20. Kusudi kubwa ya kujifunza jinsi ya kuweka nyumba yako kwenye mpangilio mzuri, ni ili kubadilisha nyumbani kwako kua sehemu takatifu, sehemu iliyobarikiwa. Wajapani wanaamini kwamba nyumba safi iliyopangiliwa kwa ufanisi inavutia Baraka, na bahati. Hivyo watu wa Japan kwao ni utamaduni kufanya nyumba kua sehemu safi, na palipopangiliwa vizuri, maana ndivyo wanavutia bahati. Ukiwa na nyumba iliyosafishwa na kupangiliwa vizuri, inavutia sana, na utakuwa unapapenda nyumbani kwako.
Asanteni sana
Tukutane wiki ijayo

Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: