Ingekuwa kuweka tu malengo ndio kuyafikia, dunia ingekuwa na watu wengi sana ambao wana mafanikio makubwa.
Lakini hali haipo hivyo, ni sehemu ndogo sana ya watu ambao wamefanikiwa.
Kwa nini inatokea hivi? Je kuna wenye bahati na wengine wenye kisirani? Kama hii ni moja ya sababu zako, basi tatizo ni kubwa kuliko nilivyofikiri.

KILICHOSIMAMA KATI YAKO NA MALENGO YAKO NI KAZI KUBWA YA KUFANYA, JE UPO TAYARI KUIFANYA?
KILICHOSIMAMA KATI YAKO NA MALENGO YAKO NI KAZI KUBWA YA KUFANYA, JE UPO TAYARI KUIFANYA?

Sawa, kila mwanzo wa mwaka watu huwa wanaweka malengo makubwa, lakini haichukui muda mrefu kabla hayajasahaulika.
Kila mtu anayeingia kwenye kazi mpya huwa anakuwa na mipango mikubwa kwenye kazi ile na anakuwa na moyo wa kuitekeleza, ni muda mchache baadaye anasahau kabisa mipango ile.
Kila mtu anayeingia kwenye biashara mpya anakuwa na mipango mizuri sana, ya kuleta mabadiliko makubwa kupitia biashara ile. Muda mchache baadaye anajikuta akiwa pale pale bila ya kufikia mafanikio aliyotarajia.
Watu wengi wamekuwa wakianzisha vitu vipya kwenye maisha yao, labda nitaanza kufanya mazoezi, lakini siku chache baadaye anashindwa. Labda nitaanza kuandika lakini siku sio nyingi anaacha.

SOMA; Ni Bora Kuweka Malengo Makubwa Na Kushindwa Kuliko Kuweka Malengo Madogo Na Kushinda.
Kwa nini hali hii?
Kwa sababu mara nyingi watu wanakuwa na mipango mizuri, ila inakuwa haiendani na vitendo walivyonavyo, au walivyo tayari kuviweka.
Mipango mikubwa inahitaji matendo makubwa na mabadiliko makubwa sana kwenye maisha, kitu ambacho wengi hawapo tayari kufanya. Na hivyo hujikuta wakiishia njiani.
Ufanye nini?
Unapoweka malengo na mipango yako, usiweke tu kujifurahisha, au kufurahisha wengine, weka na jiulize ni matendo gani natakiwa kufanya hapa, yaorodheshe, kisha jiulize, je nipo tayari kufanya yote haya.
Unapoweka malengo makubwa, ili usiishie njiani na baadaye kujiona wewe huwezi, una hatua mbili z akuchukua;
Kwanza ongeza matendo yako yaendane na mipango yako, hapa ni lazima ujitoe na kwenda hatua ya ziada.
Au kupunguza mipango yako iendane na matendo ambayo uko tayari kuyafanya.
Kama ilivyo kila kitu kwenye maisha, uchaguzi upo juu yako, chagua kile kilicho bora kwako, ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

TAMKO LA LEO;
Nimekuwa naweka malengo na mipango mikubwa na kushindwa kuifikia. Nimegundua nakuwa naweka malengo bila ya kutafakari ni hatua kiasi gani natakiwa kuchukua. Kuanzia sasa kabla sijaweka malengo makubwa, nitatafakari ni hatua kiasi gani natakiwa kuchukua, na nitaamua kuongeza matendo yangu au kupunguza malengo yangu. Lakini kwa sababu mimi ni mwana mafanikio, nitakuwa tayari kuongeza matendo yangu ili yaweze kuendana na mipango yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.