Mpendwa rafiki yangu,

Wahenga wanasema mtoto ni malezi. Changamoto kubwa ya wazazi karne ya ishirini na moja ni malezi bora ya watoto na siyo bora malezi.

Jinsi ya kumlea mtoto katika dunia yenye mtazamo hasi kwenda  katika mtazamo chanya.  Kama watu wanavyoweka kazi katika mambo mengine vivyo hivyo wanatakiwa kuweka kazi katika malezi ya watoto. Tukiwa na watoto bora tunapata jamii iliyo bora na tukiwa na jamii iliyo bora basi kwa ujumla tumekuwa na taifa bora.

Kila mmoja wetu amekulia malezi tofauti hivyo basi, ninakwenda kukushirikisha nguzo nne za malezi bora kwa watoto wetu. nguzo nne za malezi bora ni kama ifuatavyo;

Familia, kwanza ni bahati nzuri sana kila mmoja wetu kuzaliwa katika familia. Katika familia ndiyo kuna chimbuko la malezi na malezi ambayo anapata mtoto hapa yanatoka katika misingi ya watu wawili. Watoto wanapata malezi bora kutoka kwa baba na mama, wazazi wanakuwa wanawalea watoto vizuri na kuwafundisha maadili na misingi mbalimbali ya maisha.

malezi bora
silhouette of parents and their children on the beach

Wazazi wakiwa vizuri katika malezi katika ngazi ya familia basi mtoto atakuwa vizuri. Ngazi ya familia ndiko mahali ambako kuna msingi wa malezi ya watoto. Kila familia ikijitoa vizuri kuhakikisha inajenga misingi ya malezi bora basi tutapunguza matatizo mengi. Kama mzazi hana misingi anayoishi ni ngumu kwake kumshirikisha mtoto wake hivyo kama mzazi unatakiwa uwe na misingi ya kumshirikisha watoto wako.

Dini, tunapoongelea dini basi hapa tuna maanisha zile imani ambazo watu wanaaziamini hivyo na kwa kawaida watu wengi wanaimini katika misingi ya dini. Hivyo nyumba zetu za ibada kama vile misikiti na makanisa yanatusaidia sana kuwafundisha watoto malezi bora kwa mfano, watoto wengi wadogo wenye imani ya dini ya kikristu na kiislamu wanakuwa wanafundisha mafundisho katika nyumba zao za ibada. Kwa mfano, waislamu wanayo madrasa na wakristu wanayo mafundisho pia kama vile kipaimara nk.

SOMA; Jukumu Kubwa La Mzazi Katika Familia

Taasisi za kidini zinatusaidia kumlea mtoto katika malezi bora. Karibu imani zoteza kidini zinasimamia haki na upendo hivyo sina shaka juu ya imani zetu za kidini pale zinapojitoa kuwakarabati watoto katika malezi bora.

Shule, kila mmoja wetu ameiptia yule na huwa shule kuna adhabu ambazo mtu ukienda kinyume lazima mtoto aadhibiwe. Ndiyo maana wazazi wengi kitu cha kwanza wanachoangalia shule je kuna mazingira salama, mazuri na malezi bora kwa mtoto? Watu wanaangalia shule kuwa ni sehemu moja wapo ambayo inawafundisha watoto malezi bora lakini pia nidhamu na misingi ya maisha. Mtoto asipofunzwa nyumbani basi shule inachukua jukumu la kuhakisha mtoto anaendana na mfumo mzima wa shule.

Watu wengi wamebadilika kupitia taasisi za shule hata kama wazazi nyumbani walikuwa wanazembea katika kumuonesha mtoto nidhamu lakini wakiingia shule wananyooka wao wenyewe. Kuna hata wale wazazi wengine huwa wanaenda mashuleni na kuwaambia walimu kuwa huyu mtoto sisi nyumbani ametushinda hivyo tunaomba mtusaidie. Natumaini umeshawahi kusikia au kuona wewe mwenyewe mambo yanayohusiana na hayo.

Jamii, tunaishi katika jamii hivyo jamii huwa inatufundisha mengi. Kuna mambo ambayo huwa hatufundishwi nyumbani lakini jamii huwa inatufundisha. Ndiyo maana waswahili wanasema, asiye funzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu. Kama mzazi umeshindwa kumfundisha mtoto wako malezi bora basi jamii itakusaidia kumfundisha lakini kwa adhabu kali hivyo ni bora ukajitahidi kadiri ya nafasi kumjengea mtoto wako misingi bora na siyo kuchagua dunia ikuamulie.

SOMA; Jinsi Ya Kumfundisha Mtoto Kuwa Mfikiriaji Bora Na Mwenye Uwezo Mkubwa Akili

Hatua ya kuchukua leo; mpatie mtoto malezi bora na hakikisha katika kila nafasi uliyokuwepo tumika kumsaidia mtoto anapata malezi bora.

Mwisho kabisa, bila kuwa na familia bora hatuwezi kuwa na jamii bora. Familia bora inajengwa na jamii bora hivyo tukazane kujenga familia bora.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana!