Watu wengi wamekuwa wakiweka mipango mizuri na mikubwa sana kwenye maisha yao. Ila katika utekelezaji hujikuta wanakwama.
Chanzo kikubwa cha kukwama huwa ni kutaka kufanya mambo hayo yote makubwa kwa wakati mmoja au kwa muda mfupi.
Lakini haijawahi kutokea sehemu yoyote kwenye maisha yetu mambo yakaenda haraka kama tunavyotarajia. Kila kitu kinahitaji muda.

Sasa leo nataka nikushirikishe mbinu ambayo itakusaidia kuanza safari yako ya kufikia mipango mikubwa uliyojiwekea bila ya kukata tamaa.
Mbinu hiyo ni kuwa na dhana kwamba MOJA NI BORA KULIKO SIFURI.
Ndio moja ni bora kuliko sifuri kwenye namba, na hata kwenye maisha hali iko hivyo hivyo.
Unataka kuanza biashara kubwa sana, lakini huwezi kuanzia juu, anza na mteja mmoja, ni bora kuliko kusubiri. Ukishapata mteja mmoja endelea kuongeza mwingine mmoja na mmoja tena na tena na tena. Hii ni bora kuliko kutokufanya chochote kwa kusubiri mambo yawe mazuri.
SOMA; Hatua Moja Ndogo Kila Siku Ndio Kitu Pekee Unahitaji.
Unataka kuandika kitabu, huwezi kuandika chote ndani ya siku moja. Anza na dhana kwamba moja ni bora kuliko sifuri. Na kila siku andika sura moja ya kitabu. Kama sura moja ni ndefu sana andika ukurasa mmoja, kisha endelea kuongeza moja kila siku. Itafika siku kitabu kitakuwa kimekamilika.
Unataka kuanza kufanya mazoezi, huwezi kuanza kwa kukimbia kilometa moja au zaidi ya hapo. Utachoka na kukata tamaa. Lakini unaweza kuanza na kutembea hatua chache, au kupiga push up chache, au kuruka kamba. Moja ni bora zaidi ya sifuri.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba kufanya kitu kidogo ni bora kuliko kutofanya kabisa. Kuanzia sasa nitaanza mipango yangu yote kwa hatua ndogo ndogo ambazo najua baada ya muda zitanifikisha kwenye lengo langu. Moja ni bora kuliko sifuri, nitajikumbusha jambo hili kila wakati na katika kila hali nitakayokuwa napitia. Kitu muhimu ni kuanza, vingine vitawezekana tu.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.