Mambo 8 Ya Kufanya Kama Kile Unachokifanya Hakikupi Matokeo Unayoyataka.

Kuna wakati katika maisha yako unaweza ukajikuta unafanya kila kilicho sahihi kwako ili kupata matokeo unayotaka, lakini kitu cha kushangaza matokeo hayo unakuwa huyapati. Ni kweli unaweza ukawa unafanya kazi kwa bidii, una mipango na umejiandaa vizuri, lakini kila ukiangalia bado havikuridhishi na havifanyi kazi sawasawa.
Ukweli huu unakuja kuuthibitisha mwenyewe kila unapotazama mabadiliko makubwa hayatokei ikiwa ni pamoja na kutengeneza pesa za kutosha, zaidi unajiona kama uko palepale. Kwa hali hii inapokutokea inakuwa ni rahisi sana kutaka kukukatisha tamaa.  Hiyo yote inakuwa hivyo ni kwa sababu unakuwa unashindwa kujua wapi ulipokosea kama ni uwezo wote umeuweka hapo lakini matokeo huyaoni.
Kwa hiyo kwa vyovyote vile unakuwa unaona mipango yako au kile unachokifanya kimeshindwa. Hivyo basi,  akili yako yote inakuwa inapiga sana kelele na kukuambia kuwa ni lazima kubadilisha njia nyingine kwa hili haliwezekani tena. Hali inaweza ikawa imekukuta kwa namna moja au nyingine, unapokumbana nayo unafanyaje?
Katika makala yetu ya leo nimekuwekea mambo ya kufanya kama kile unachokifanya hakikupi matokeo unayoyataka. Kwa kufanya mambo hayo yatakusaidia kuweza kuendelea mbele hata kama ulihisi umekata tamaa. Kikubwa cha kufanya ni kuweza kuyafanyia kazi ili yakusaidie kupata mwelekeo, nguvu na dira mpya ya kukufikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji.
Yafuatayo Ni Mambo 8 Ya Kufanya Kama Kile Unachokifanya Hakikupi Matokeo Unayoyataka.
1. Chukua muda kila siku kutafakari ni kwanini  hupati matokeo unayoyataka. Angalia ni wapi unapokosea hata kama kila kitu unacho kisha jirekebishe na endelea kung’ang’ania mpaka uyaone mafanikio yako.
2. Tafuta msaada kwa kupata ushauri kwa watu uliokaribu nao. Watu hao hakikisha wawe ni wale wanaofanya kile kinachoendana na wewe. Kwa ushauri wao watakupa uzoefu wao ambao utakusaidia kuendelea kusonga mbele kwa mtindo tofauti badala ya kuacha.
3. Kuwa makini na watu wanaokuzunguka katika kipindi hiki. Ni rahisi wakakukatisha tamaa na kukwambia wewe tena ndiyo basi huwezi tena. Kwa maneno yao unaweza ukaamini na ukachukulia huo ndiyo ukweli na ukajikuta umekwama.
4. Badili mipango yako upya jinsi ya kufanya hicho kitu ulichokuwa ukikifanya kwa namna ya tofauti tena. Ukibadili hiyo mipango na kuboresha zaidi katika maeneo mengine unaweza ukapata matokoe uliyokuwa ukiyahitaji kwako hapo mwanzo.
5. Badili mipango yako upya jinsi ya kufanya hicho kitu ulichokuwa ukikifanya kwa namna ya tofauti tena. Ukibadili hiyo mipango na kuboresha zaidi unaweza ukapata matokoe uliyokuwa ukiyahitaji kwako hapo mwanzo.
6. Chukua muda kiasi wa kukaa chini na kutuliza akili yako na kufanya tahajudi (Meditation) ili kuipa akili yako nguvu zaidi ya kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa.
7. Kama ulikuwa ni mtu wa kufanya mambo mengi ni bora ukabadili mwelekeo wako na kuanza kuweka nguvu na uwezo wako wote kwenye kitu kimoja mpaka kikupe matokeo chanya unayoyahitaji.
 8. Kumbuka mafanikio hayaji tu kwa urahisi wakati mwingine yanakuja kwa kutumia kanuni ya ung’ang’anizi. Hivyo basi ng’ang’ana mpaka upate matokeo unayoyataka. Inapotokea mambo yamegoma jaribu tena na tena mpaka mlango wa mafanikio utafunguka.
Kuwa tayari kubadilika na kufanyia kazi mambo hayo muhimu ili kubadili hatima ya maisha yako. Hata hivyo kama kitu hicho ni kweli unaona kabisa huwezi kukibadli basi ni vyema ukaangalia namna nyingine ya kufanya ambayo itakuwa nafuu kwako kuliko kung’ang’ania sana ambako kunaweza pengine kukupeleka kubaya.
Tukutakia ushindi katika safari ya mafanikio yako na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza na kuhamasika kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri karibu pia katika DIRA YA MAFANIKIOkujifunza na kuboresha maisha.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 048035,

dirayamafanikio@gmail.com.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: