Hofu na moto ni vitu ambavyo vinafanana sana. Vyote vina faida kubwa sana na vyote pia vina hasara kubwa.

Tuanze na moto..

Moto ni mzuri sana, tunatumia moto kupikia, tunautumia kupata joto, kuchemsha maji na mengine mengi. Lakini moto huu ni hatari sana, unaweza kuteketeza nyumba na vitu vyote. Lakini pamoja na haya bado hatujaacha kutumia moto, tunauheshimu na kuutumia vizuri.

Hofu nayo iko hivyo hivyo inaweza kuunguza kabisa mawazo yako mazuri ya kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako.

LICHA YA KUWA NA HOFU, ENDELEA KUFANYA.
LICHA YA KUWA NA HOFU, ENDELEA KUFANYA.

Unafanya nini sasa?

Itumie hofu kama kitu kinachokupa taarifa. Unapokuwa na hofu jua ya kwamba unakaribia kufanya kitu ambacho hujazoea kufanya au ambacho huna uhakika nacho. Tumia hofu kama taarifa na hivyo kuchukua tahadhari zaidi. Lakini usikubali hofu ndio ikuongoze wewe, usikubali hofu ikuzuie kuchukua hatua.

SOMA; Kama Huna Hofu, Una Tatizo Kubwa Sana.

Kwa kifupi unapokuwa na hofu iambie hivi; hofu nimekuelewa na sasa nasonga mbele. Huku ukiwa umeshachukua tahadhari zitakazo zuia kile unachohofia kisitokee.

TAMKO LANGU;

Nimejua hofu ni sehemu muhimu ya kunipa taarifa juu ya kile ninachofanya. Hofu ni hatari kama moto, nisipokuwa makini nayo inaweza kuunguza kabisa mipango yangu mizuri. Hivyo kuanzia sasa nitakapopata hofu nitachukulia kama taarifa muhimu juu ya kile ninachofanya. Nitaiambia hofu nimekuelewa na sasa nasonga mbele huku nikiwa na maandalizi ya kutosha juu ya kile ambacho nahofia.

NENO LA LEO.

To overcome a fear, here’s all you have to do: realize the fear is there, and do the action you fear anyway.

Peter McWilliams

Kama unataka kuishinda hofu fanya hivi; tambua kwamba kuna kitu unahofia na fanya hiko kitu unachohofia kufanya.

Rafiki na Kocha Wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.