Mbinu Kumi(10) Za Kuwafanya Wateja Waendelee Kufanya Biashara Na Wewe.

Kazi kubwa sana unayohitaji kufanya baada ya kumpata mteja ni kuhakikisha anaendelea kuwa wako, yaani anaendelea kufanya biashara na wewe.
Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwafikisha wateja kwenye biashara zao, lakini wateja wanapofika na kupata huduma huondoka na wengi kutokurudi tena.
Ni rahisi sana kumuuzia mteja ambaye ulishamuuzia awali, kuliko kumuuzia mteja mpya. Hivyo kama ukiweza kuiendesha biashara yako vizuri, wateja ambao wananunua kwako watakuwa wateja wako wa kudumu.
NAPENDA BIASHARA
Zifuatazo ni mbinu kumi unazotakiwa kuanza kuzitumia leo kwenye biashara yako ili kuhakikisha wateja wako wanaendelea kufanya biashara na wewe.
1. Tekeleza ulichoahidi.
Kama umemtangazia mteja kwamba akija kwenye biashara yako atapata kitu fulani, basi hakikisha anapata kitu hiko. Hakuna kitu ambacho watu hawapendi kama kudanganywa. Mteja anapoona kwamba amedanganywa hatorudi tena kwenye biashara yako na utakuwa umemkosa milele. Hakikisha unatimiza ulichomwahidi mteja wako.
2. Ahidi kikubwa na pitiliza(overpromise and overdeliver)
Najua hapa unaweza usielewe kwa sababu ulichozoea ni kuahidi kidogo na kupitiliza(underpromise and overdeliver). Hii ilikuwa unafanya kazi zamani, ila kwa sasa, haifanyi kazi tena. Kwa sababu kama wewe unaahidi kidogo, wenzako wanaahidi kikubwa na wanafanyia kazi. Hivyo kitu pekee cha kuhakikisha unawabakisha wateja ni kuwaahidi makubwa na kuyapitiliza hayo. Kama umejitoa kweli kwenye biashara yako, hili halitakushinda.
3. Imarisha mawasiliano yako na wateja wako.
Ni muhimu sana uwe na mawasiliano na wateja wako. Bila ya kujali ni biashara gani unafanya, kuna na mfumo w akupata namba za simu, au barua pepe za wateja wako. Mata kwa mara watumie ujumbe ukiwatakia heri na wakati mwingine kuwajulisha bidhaa au huduma mpya zilizopo kwenye biashara yako.
4. Fanyia kazi malalamiko ya wateja haraka.
Wateja wanapokuwa na malalamiko, yafanyie kazi haraka sana. Usisubiri mpaka yawe makubwa kiasi cha kuwafanya watafute mahali pengine wanakoweza kufanya biashara bila ya matatizo wanayopata kwako.
5. Toa huduma bora ambazo mteja hawezi kupata popote.
Huduma kwa wateja, mteja amepokelewaje, ameelezwaje kuhusiana na bidhaa au huduma anayohitaji, maswali yake yamejibiwaje, hivi ni vitu vinavyoonekana vidogo sana ila vina maana kubwa sana kwa wateja wa biashara yako. hakikisha wateja wako wanapata huduma ambazo zitawafanya wajisikie ufahari.
SOMA; Dalili Tatu(3) Kwamba Biashara Yako Inahitaji Mabadiliko Ya Haraka.
6. Wakumbuke wateja waliopotea.
Kama biashara yako imekuwepo kwa muda, kuna wateja waliokuwepo awali ila kwa sasa hawapo tena. Kuna wateja ulikuwa unafanya nao biashara zamani, ila kwa sasa huwaoni tena kwenye biashara yako. ni vyema kuwatafuta na kujua kwa sasa biashara wanafanya na nani na ni kitu gani limewafanya hawaji tena kwako.
Kusoma mbinu nne zilizobaki bonyeza maandishi haya na uendelee kusoma.
Makala hii inatoka kwenye mtandao wa NAPENDA BIASHARA, mtandao bora kabisa wa kukupatia wewe maarifa ya kufanikiwa kwenye biashara. Utembelee kila siku kwa kwenda www.napendabiashara.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: