Watu wengi wamekuwa wakifikiria njia bora ya kuwa kile wanachotaka kuwa.
Njia bora ya kuingia kwenye biashara, njia bora ya kufanya kazi, njia bora ya kusoma, njia bora ya kuwa na maisha bora.
Unaweza kufikiri sana hili, unaweza kujifunza sana, unaweza kuweka malengo na mipango mizuri.
Lakini haya yote hayatakuletea ile njia bora unayotafuta.
Njia bora kwako ni kufanya..
Unafikiria njia bora ya kuingia kwenye biashara? Anza kufanya biashara hiyo unayotaka. Ndio anza sasa na anzia hapo ulipo, usiseme unasubiri kujipanga au uwe tayari. Hutakuwa tayari zaidi ya ulivyo leo.
Unataka njia bora ya kufanya kazi zako vizuri, anza sasa kuzifanya kwa ubora, hakikisha unaleta tofauti, unaongeza thamani na kazi yako inakuwa bora kweli.
Unataka njia bora ya kuwa na maisha mazuri? Anza kuishi maisha yako, anza kufanya kile ambacho unapenda kweli kukifanya. Anza kuishi kulingana na kile unachoamini ni sahihi na sio kile ambacho kila mtu anamuiga mwenzake.
Chochote unachotaka, anza kufanya. Unaweza kuwa na maandalizi utakavyo, unaweza kuomba ushauri kwakila mtu na unaweza kuwa na subira utakavyo, ila hutayapata matunda kama hutaanza kufanya.
Kuna kitu unataka? Anza kufanya.
SOMA; Mambo 10 Rahisi Unayoweza Kuanza Kufanya Leo Na Ukaboresha Maisha Yako.
TAMKO LANGU;
Najua chochote ninachotaka kwenye maisha yangu naweza kukipata kama tu nitakuwa tayari kukifanya. Najua kufanya ndio njia pekee ya kupata kile ambacho nimekuwa nakifikiria sana. Kuanzia sasa nitakuwa mtu wa kufanya zaidi ya kuongea na kusubiri mpaka kila kitu kiwe sawa. Kwa sababu najua hakuna wakati ambapo vitu vyote vitakuwa sawa.
NENO LA LEO.
The man who goes alone can start today; but he who travels with another must wait till that other is ready, and it may be a long time before they get off.
Henry David Thoreau
mtu anayeenda mwenyewe anaweza kuanza leo; lakini mtu anayeenda na mwingine ni lazima asubiri mpaka mwenzake awe tayari, na inaweza kuwa ni muda mrefu sana mpaka waje kuanza safari.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.