Kuwa bize na kuzalisha ni vitu viwili tofauti kabisa.
Mara nyingi wale wanaoonekana kuwa bize sana huwa wanakuwa na uzalishaji mdogo sana, japo wao wanaweza kufikiri kinyume chake.
Kila mtu anaweza kuwa bize, lakini ni wachache sana wanaoweza kuwa na uzalishaji mkubwa.
Unaweza kuwa bize kwa kufanya mambo ambayo hayana mchango mkubwa kwako na kwa mafanikio yako. ila unapopima uzalishaji, unapima kile hasa ulichofanya ambacho kinakusogeza mbele zaidi.
Lengo la makala hii ya leo sio wewe uache kuwa bize na uwe mvivu, bali ni wewe uache kukazana na ubize na badala yake ukazane na uzalishaji. Je ni kiasi gani umezalisha? Je ni wapi unaweza kuboresha zaidi?
Sehemu kubwa ya mambo yanayokuweka bize, sio muhimu sana kwako kiasi kwamba hata usingeyafanya bado maisha yako yangeendelea kuwa bora. Na hata kama kuna ambayo ni muhimu basi kuna wengine wangeweza kuyafanya vizuri na wewe ukabaki na muda w akutosha kufanya yale ambayo ni muhimu kwako.
Kama unataka kufikia mafanikio makubwa unayotazamia, acha kujipima kwa ubize na anza kujipima kwa kile unachozalisha.
SOMA; Acha Kutafuta Pesa Ambazo Hutazipata, Tafuta Hiki Kimoja Na Usahau Matatizo Yako Ya Pesa.
TAMKO LANGU;
Nimejua ya kwamba kuwa bize sio sawa na kuzalisha, na mafanikio hayatokani na kiasi gani mtu yupo bize, bali ni kiasi gani mtu anazalisha. Kuanzia sasa naacha kukazana na ubize na badala yake nakazana na uzalishaji. Nakazana na yale ambayo ni muhimu sana kwangu ili niweze kufikia mafanikio makubwa. Mengine yote naachana nayo.
NENO LA LEO.
Productivity is never an accident. It is always the result of a commitment to excellence, intelligent planning, and focused effort.
Paul J. Meyer
Kuwa na uzalishaji bora sio ajali. Mara zote ni matokeo ya kujitoa kufanya kwa ubora, kupanga vizuri na kupeleka nguvu zote kwenye kile unacofanya.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.