Kama umekutana na changamoto au kikwazo….
Na ukaweka juhudi zako zote katika kutatua changamoto au kuvuka kikwazo hiko,
Lakini kila kitu kikashindikana,
Kuna dawa moja ya uhakika imebaki.
Na dawa hiyo ni muda.
Mwisho wa siku muda ni tiba nzuri sana kwa changamoto au kikwazo chochote.
Kama utaendelea kukomaa na hutokata tamaa, kadiri muda unavyokwenda, utapata suluhisho au changamoto ile itapotea yenyewe.
Hivyo hata kama unaweka juhudi kubwa lakini huoni matokeo mazuri, kamwe usikate tamaa, muda utatibu yote hayo.
ANGALIZO; Elewa vizuri hili, usiendelee kuteseka kwa mateso unayopewa na mtu ukiamini kadiri muda unavyokwenda atabadilika, huwezi kuwa na uhakika na hilo.
SOMA; Jinsi ya kutengeneza bajeti ya matumizi mazuri ya muda wako kama mjasiriamali.
TAMKO LANGU;
Najua ya kwamba pale ninapokutana na changamoto kubwa, na juhudi zangu zote zikashindwa kutatua, kitu pekee kinachoweza kunisaidia ni muda. Muda ni rafiki mzuri na hakuna changamoto inayoweza kuushinda muda. Mimi nimeamua sitokata tamaa kwenye jambo lolote ninalolifanya, hata kama mambo ni magumu kiasi gani, najua muda uko upande wangu.
NENO LA LEO.
“Some people stand by you in your darkest hour, while others walk away; only a select few march toward you and become even closer friends.”
― Jeffrey Archer
Mambo yako yanapokuwa magumu, kuna baadhi ya watu wataendelea kusimama na wewe na wengine wengi watakuacha, ni wachache sana ambao watakuja kwako, na hawa ndio watakuwa marafiki wa kweli.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.