Wewe kama mwana mafanikio, ni lazima mpaka sasa uwe unajua ya kwamba hakuna kitu ambacho kinapatikana kirahisi tu. Kila kitu kina changamoto zake, na vikwazo vyake pia.
Hata uwe umejiandaa vipi, bado utakutana na changamoto, hii ni njia ya maisha.
Pamoja na changamoto hizi bado unahitaji kushinda, na utaweza kushinda vizuri sana, kama utajua vizuri kuhusu changamoto hizi.
Huwezi kuchagua ni changamoto gani ije kwako, changamoto itakuja, iwe ni kubwa au ndogo, ya kawaida au mbaya sana, huwezi kuchagua.
Lakini kuna kitu kimoja muhimu sana unachoweza kuchagua, kwa kukijua hiki utaweza kuvuka kila changamoto na hatimaye kufikia mafanikio.
Kitu pekee unachoweza kuchagua ni unazichukuliaje changamoto unazokutana nazo. Kuna ambao wanazichukulia kama sehemu ya kujifunza na hivyo wanajifunza na kusonga mbele. Kuna ambao wanachukulia kama ndio mwisho wa safari na hivyo wanakata tamaa kabisa.
Je wewe unazichukuliaje changamoto? Unachukua hatua gani unapokutana na changamoto? Hiki ni kitu ambacho unaweza kuchagua wewe mwenyewe, na kutokana na utakavyochagua utaweza kwenda mbele zaidi au unaweza kupotea kabisa.
Chagua kuichukulia kila changamoto kama sehemu ya kujifunza na moja ya njia za kufikia mafanikio makubwa, na utaona fursa nyingi sana za kufikia mafanikio hayo.
SOMA; MAMBO 20 NILIYOJIFUNZA KWENYE KITABU HOW TO STOP WORRYING AND START LIVING.
TAMKO LANGU;
Nimejua ya kwamba siwezi kuchagua ni changamoto gani ije kwangu, ila nina uwezo wa kuchagua ni jinsi gani nachukulia changamoto ninazokutana nazo. Hata changamoto iwe kubwa kiasi gani, haiwezi kunizuia kama mimi mwenyewe sijakubali inizuie. Kuanzia sasa nachagua kuichukulia kila changamoto kama sehemu ya kujifunza na njia ya kufikia mafanikio makubwa zaidi. Changamoto sio mwisho wa safari yangu.
NENO LA LEO.
What really frightens and dismays us is not external events themselves, but the way in which we think about them. It is not things that disturb us, but our interpretation of their significance.
Epictetus.
Kinachotuogopesha na kutusikitisha sio mambo yanayotokea, bali jinsi tunavyoyafikiria mambo hayo. Sio kitu kinachotokea kinatusumbua, bali tafsiri yetu kwa kitu hiko ndio inayotusumbua.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TUPO PAMOJA.