Huyu Ndiye Mtu Anayekuzuia Kufikia Mafanikio Makubwa, Na Jinsi Ya Kumshindwa.

Najua umekuwa unakazana kuweka juhudi kubwa sana ili kuweza kutoka hapo ulipo sasa na kwenda mbali zaidi.
Najua umekuwa unakazana sana ili uweze kufikia mafanikio makubwa ambayo umedhamiria kwa muda mrefu.
Lakini pamoja na juhudi zote hizi kubwa bado huoni ukipiga hatua, bado unaendelea kuwa pale pale na huoni dalili za kufikia mafanikio makubwa unayotarajia.
Kwa nini sasa uishie kwenye hali hii licha ya kuweka juhudi kubwa?
Haiwezekani, lazima kutakuwa na mtu.

UMEJIFUNGIA BOMU LAKO MWENYEWE, NA KAMA USIPOSTUKA, LITAKULIPUKIA.

 
Jibu rahisi na la uhakika ni kwamba kuna mtu anakuzuia wewe kuweza kufikia yale mafanikio ambayo umepanga na kujitoa kuyafikia. Ndio ninakuhakikishia kabisa ya kwamba yupo mtu, vinginevyo zoezi la wewe kufikia mafanikio lisingekushinda, mbona wengine waweze ila wewe tu ndio ushindwe?
Na mimi nakubaliana na wewe kabisa ya kwamba kuna mtu anakuzuia. Na najua ya kwamba umekuwa hujamjua mtu huyo vizuri, au huenda umekuwa na hisia lakini huna uhakika kabisa na mtu huyo.
Sasa leo kwenye makala hii, nakwenda kumfunua mtu huyu, umjue kwa undani na jinsi ambavyo amekuwa anakuwekea vikwazo ili usifanikiwe. Na baada ya kumjua nitakwenda kukushirikisha njia bora za kuweza kumshinda mtu huyu ili uweze kufikia malengo yako makubwa uliyojiwekea kwenye maisha.
Je upo tayari?
Upo tayari kumjua mtu ambaye amekuwa anakurudisha nyuma, mtu ambaye amekosa huruma, licha ya kukuona unaweka juhudi hizo bado anakurudisha nyuma? Kama ndio basi karibu sana umjue mtu huyu. Na pia ujue dawa yale ili asiendelee kukuzuia.
Mtu ambaye amekuwa anakuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa, ambaye amekuwa anaweka vikwazo kwenye njia zako za kukufikisha kwenye mafanikio, ni huyu hapa; NI WEWE MWENYEWE.
Ndio wewe mwenyewe umekuwa adui yako mkubwa sana, wewe mwenyewe umekuwa unajihujumu, huku unaweka jitihada, huku unaharibu jitihada hizo. Na umekuwa unafanya hivi miaka nenda miaka rudi bila hata ya kujua.
Na kama hutaendelea kujifunza hapa ka makini, kama utaishia kusema nilijua tu halafu ukaondoka, utaendelea kufanya makosa ambayo umeyafanya tangu umepata akili mpaka leo, na makosa hayo yataendelea kukugharamu kama hutajifunza leo hatua za kuchukua
SOMA; Akili Ni Nywele Kila Mtu Ana Zake, Je Unamjua Adui Wa Akili Yako?
Unakuwaje adui yako mwenyewe?
Unaweza kusema Kocha mimi sikuelewi kabisa, yaani pamoja na kwamba nimeweka malengo na ninayafanyia kazi, inawezekanaje nikawa adui yangu mwenyewe? Pamoja na kwamba nafanya kazi kuliko wengine, naweka akiba na kuwekeza, inawezekanaje niwe adui yangu mwenyewe? Usiwe na haraka, twende taratibu tujifunze na baadae utapata nafasi ya kuchukua hatua.
1. Unaendelea kubaki na mawazo hasi.
Pamoja na kuamua ya kwamba unataka kufikia mafanikio makubwa, pamoja na kujitoa kuweka juhudi kubwa ili kufikia mafanikio unayotaka, bado umekuwa unaruhusu mawazo hasi yaingie kwenye akili yako. na hii imekuwa sumu kubwa sana kwako.
Kwa njia hii uliyochagua, wazo moja hasi linafuta mawazo mazuri 100. Kwa mfano unajua kabisa ya kwamba ni lazima utakutana na changamoto, na pale changamoto inapokuja unafanyaje? Unapaniki, unaanza kufikiria kama mambo yatakwenda vibaya itakuwaje, vipi kama utashindwa? Na mengine mengi. Na kwa mawazo haya hasi ni nini kinatokea? Unakaribisha hali ile hasi na pia ni rahisi kukata tamaa.
Mawazo mengine hasi ni kuwaonea wengine wivu, kujaribu kushindana na wengine na pia kulaumu au kulalamika.
Safari hii uliyochagua haitaki wazo hasi hata moja kwenye akili yako, ni sumu kali sana inayoweza kuua mambo makubwa ambayo ungeyapata.
Kama kweli unataka kupiga hatua, kama kweli unataka kufikia mafanikio makubwa, basi huna budi kuachana kabisa na mawazo hasi. Mawazo hasi hayana faida yoyote kwako zaidi ya kuwa mzigo, na kukugeuza wewe kuwa adui yako mwenyewe.
2. Kuendelea na tabia za awali.
Kabla hujabadili gia ya maisha yako, na kuamua kuishi maisha ambayo yatakufikisha kwenye malengo yako, kuna tabia ambazo ulikuwa nazo. Na sehemu kubwa ya tabia hizi haziendani na hali ya mafanikio unayotaka kuyatengeneza.
Lakini wewe umeamua kuacha tabia hizi ziendelee kuwepo kwako. Ukiamini ya kwamba tabia hizi hazina tatizo lolote kwako kufikia malengo yako. hapa ndio umekuwa unajidanganya na umekuwa adui wako mwenyewe.
Kama una tabia yoyote ambayo haiendani na hali ya mafanikio unayotengeneza, tabia hii ni kikwazo kwako kufikia malengo yako. ni lazima uweze kuondokana na tabia hizo mara moja ili uondoe vikwazo kwenye njia yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Ndio tabia ni ngumu sana kubadili hasa pale ambapo umeishi nazo kwa muda mrefu. Ila unaweza kuanza na mabadiliko madogo madogo na baada ya muda ukajikuta umeshabadili tabia zako zote mbaya.
3. Kuendelea kuruhusu maoni ya wengine kuongoza maisha yako.
Kabla hujaianza safari hii ya mafanikio, ulikuwa umeruhusu kila mtu aweze kukuathiri na maoni yake. Watu wakisema biashara fulani inalipa, basi na wewe unaondoka hapo na kwenda kuianza, kwa sababu watu wanasema inalipa. Unapoanza kitu kikubwa na watu wakakuambia huwezi au utashindwa, ulikuwa unaacha kwa sababu watu wamesema huwezi, utashindwa.
Sasa umeianza safari ya mafanikio, umejitahidi kupunguza kusikiliza maneno ya watu, lakini bado hujakata kabisa huo mzizi.
Kama kweli unahitaji kupiga hatua kuelekea kule unakotaka, ni lazima ukate kabisa huu mzizi wa kukubali maamuzi yako yaamuliwe na maoni ya wengine.
Hii haimaanishi kwamba unawazuia watu wasitoe maoni yao, bali unawaacha wayatoe, lakini wewe unajua ni maoni tu na hulazimiki kwa njia yoyote ile kuyatumia au kuyafuata, hata kama yametolewa na mtu wa aina gani.
Ni lazima ujue ya kwamba wewe ndio mwamuzi wa mwisho wa maisha yako na maamuzi yoyote utakayochukua uwe tayari kuyasimamia.
SOMA; Mambo 6 Yanayokukwamisha Na Kukurudisha Nyuma Sana Katika Maisha Yako.
Njia ya uhakika ya kukabiliana na adui huyu.
Mpaka sasa umeshamjua adui yako si ndio? Unakubali kwamba wewe ni adui yako mwenyewe? Unakubali kwamba moja kati ya vitu hivyo tulivyojadili hapo juu huwa vinakutokea? Kama ndio basi karibu hapa upate dawa ya adui yako huyu.
Kwenye kujadili hapo juu tayari nimekuambia uwe chanya, ubadili tabia, na pia usikubali maoni ya wengine ndio yawe maamuzi yako. lakini najua huenda umeshajaribu lakini umeshindwa. Najua kusema au kuandika ni rahisi kuliko kutenda.
Je nikikuonesha njia unayoweza kutumia na ukapata majibu ya uhakika kwenye maeneo hayo matatu utaichukua njia hii? Kama jibu ni ndio basi njia ni hii hapa;
Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kisima cha maarifa ni blog ambayo ina makala nzuri sana za jinsi ya kujijengea tabia za mafanikio, makala za tabia za watu wenye mafanikio, makala za kujijengea mtazamo chanya kila siku. Ili kupata nafasi ya kusoma blog hii unahitaji uwe mwanachama uliyejiunga na kulipa ada ya mwaka.
Pia kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la wasap ambapo utapata nafasi kubwa ya kujifunza zaidi.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada ya uanachama wa mwaka mmoja ambayo ni shilingi za Tanzania elfu hamsini(50,000/=). Lipa ada hii kwa namba zifuatazo, tigo pesa 0717396253 au mpesa 0755953887 kisha tuma taarifa zako kwenye namba hizo na utapewa maelekezo zaidi.
Usikose nafasi hii ya kipekee kwako kuweza kupambana na adui mkubwa sana wa maisha yako ambaye ni wewe mwenyewe.
Leo fikia azimio la kummaliza kabisa adui huyu ambaye amekuwa anakuzuia, na anza kufanyia kazi haya uliyojifunza.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
AMKA CONSULTANTS.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: