Kwanza kabisa, kabla hatujachanganyana, unapoanza biashara, anza na biashara ambayo wateja wako tayari kununua. Hivyo ni lazima ujue matatizo ambayo watu wanayo na uje na suluhisho.

Sasa pamoja na kuwa na kitu ambacho watu wanataka, bado usimpe mteja kile ambacho anataka yeye, bali mpe kile ambacho ni bora zaidi.

Mteja anapokuja kwako anakuwa na matarajio fulani, kutokana na huduma uliyowahi kumpa hapo mwanzo au kama ni mteja mpya basi kutokana na uzoefu alionao kupitia wafanyabiashara wengine.

Sasa wewe usitoe kile ambacho mteja anategemea kupata, bali toa kilicho bora zaidi. Hata kama unauza bidhaa ambayo tayari mteja anaijua, basi mpe huduma bora sana ambazo hajawahi kupata sehemu nyingine yoyote.

Na kama biashara yako inahusisha huduma za kitaalamu, mteja anaweza kuja kwako anataka kitu fulani, na kama ukifanya kama anavyotaka yeye ni chini ya viwango vyako, hapo mshawishi mteja apokee kile kilicho bora zaidi.

Kumbuka jina lako linaandikwa kwenye kitu chochote unachofanya, usikubali jina lako liandikwe kwenye kitu ambacho sio bora sana.

Mpe mteja kilicho bora sana na utakuwa na uhakika wa kupata wateja wengi na wa kudumu.

MUHIMU; Kama una swali, maoni au changamoto yoyote ya kibiashara, weka kwenye maoni hapo chini na tutajadiliana zaidi na kama itahitajika nitaandaa makala ya kuhusu jambo hilo kwenye makala zijazo.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz