Kama Unataka mabadiliko Makubwa, Anza Kubadili Kitu Hiki Kwanza.

Hii sio siri sasa, bali ni ukweli ulio wazi kuwa kila mtu anapenda mabadiliko makubwa katika maisha yake. Ndiyo maana hata moyoni mwako ukijichunguza wewe mwenyewe, utagundua  unapenda mabadiliko na mafanikio, lakini bado unajiuliza hivi nitapata wapi mabadiliko kwenye maisha yangu?
Mmh! Usivyo hata na upendo wa maisha yako mwenyewe ati unajidanganya ‘oh! Mimi siwezi, sio kipaji changu’ na unabaki kutoa sababu kuwa wazazi ndio chanzo, umekata tamaa na zaidi ya yote bila hata wasiwasi kila siku unabaki kusema ‘Maisha ni magumu’.
Ni kweli maisha yanaweza yakawa magumu kama unavyosema sikukatalii, lakini kitu unachotakiwa ujiulize nani aliyekuahidi maisha ni rahisi? Nani aliyekwambia ati ukipata kazi nzuri ndio basi kila kitu kimeisha? Au ni nani aliyekwambia ukipata pesa ndiyo unaweza kufanya mabadiliko yoyote unayotaka?
Haya ngoja nikuulize wewe mwenyewe kwanza. Ni wangapi wanapesa na hawana hata punje ya mabadiliko makubwa zaidi wanaishi maisha yaleyale, nyumba ni ileile, matatizo ni yaleyale. Ni wangapi wanapokea mishahara mizuri lakini baada ya muda mfupi hata hawajui pesa zilipoelekea.
MABADILIKO MAKUBWA YA MAISHA, YANAANZA NA WEWE.
Matatizo yakujitakia mwenyewe usisingizie wengine eti umefanyiwa changa la macho, usianze kumsema mtu eti amekuloga. Je, ulimwona akikuloga, unachoamini eti huna nyota na hata sasa bado unabaki kujilinganisha na wengine wala huna msimamo.
Acha kutingisha kichwa na kuangalia chini kujuta na kujihisi, wewe elewa na tambua nakueleza mabadiliko sahihi yanapotakiwa kuanzia na ufanye nini ili kuweza kuyapata mafanikio hayo siku zote za maisha yako na uache visingizio vyako . Ndiyo unaweza kupata mafanikio makubwa ukitaka.
Hauhitaji akili za ziada au kutumia nguvu nyingi sana, sababu mabadiliko hayaji tu ‘automatic’, bali mabadiliko yoyote yanaanza kiakili halafu kimwili. Kama haujajua, huu ndiyo ukweli halisi unataka mabadiliko ni lazima uanze na wewe mwenyewe kwa kuhakikisha unatoa thamani inayoendana na mabadiliko unayoyataka.
Ni sahihi kabisa ninaposema mabadiliko ni lazima yaanze na wewe mwenyewe, kama unabisha nyosha mkono juu. Huu ni ukweli usiopingika mabadiliko ni kwako mwenyewe kwanza. Ni lazima ubadilike na kutoa thamani itakayokupa mafanikio unayoyataka, bila kufanya hivyo sahau kwanza mafanikio.
Kuwa na viongozi wazuri pekee hawatoshi, kuwa na pesa ndio kabisa sio chanzo pekee cha kukufanikisha na kukupa mafanikio ya kudumu, usidanganyike. Siku zote mabadiliko yanaanza  na wewe mwenyewe, halafu ndiyo utaweza kubadilisha historia ya maisha yako na kuacha wengine wakishangaa kwa sababu walifikiria hautaweza kuja kufanikiwa.
Anza sasa, kabla ya kuangaza angaza macho sehemu nyingine. Anza kujiangalia wewe kama wewe na kutaka mabadiliko. Hiyo tabia yako anza nayo, badilisha kauli zako na tena uwe makini. Aga kabisa na usirudi tena kwenye ulevi, ugomvi usio maana. Ishi maisha chanya na kutafuta mafanikio yako.
Acha kuishi maisha yasiyokupeleka mbele kimafanikio. Penda maisha yako kwa kuishi maisha ya faida siku zote. Jifunze pia kutunza muda wako. Acha kuangalia angalia simu masaa yote wakati hakuna kikubwa unachokifanya huko. Ili kufanikiwa kitu kikubwa unachotakiwa kwanza kukibadili ni wewe mwenyewe na si kitu kingine.
Kumbuka kama nilivyoanza kusema mabadiliko makubwa yaanzia kwako. Hapa ndipo mabadiliko makubwa unayoyataka yanapoanzia. Utabaki kuona mabadiliko ya wenzako mpaka lini? Yape maisha yako thamani kwa kuanza kubadilika kwanza na utaona karibu kila kitu kinabadilika na kuwa na maisha ya tofauti.
Nikutakie siku njema na ansante kwa kutembelea AMKA MTANZANIA kwa ajili ya kujifunza.
Makala hii imeandikwa na Noel Ngowi wa Moshi- Tanzania. Kwa mawasilino zaidi na mwandishi anapatikana kwa e-mail  ngowi123@gmail.com.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s