Karibu Kwenye Chuo Kikuu Kinachotembea (University On Wheels), Jifunze Popote Ulipo.

Moja ya hitaji la msingi sana kwenye maisha yako, kama unataka kuishi maisha bora na ya mafanikio ni kujifunza. Na kujifunza huku sio kama kule kwa shuleni kwamba ukishahitimu unaweka vitabu pembeni, badala yake unahitaji kujifunza kila siku, yaani KILA SIKU.
Unahitaji kujifunza kila siku katika maeneo mbalimbali ya maisha yako, ikianzia kuhusu kuongeza ubora kwenye kazi au biashara yako, kuboresha maisha yako binafsi, kuwa na mtizamo chanya, kushawishi na mengine mengi ambayo ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio.
Lakini changamoto inakuja moja, sina muda wa kujifunza kila siku, ratiba zangu zimebana sana, kazi au biashara zangu zinanichukua muda mrefu wa siku, nikitoka nimechoka na siwezi kushika kitabu nisome. Hii ni sababu ambayo imewafanya wengi kushindwa kujijengea tabia ya kujifunza kila siku.
Leo nina habari njema kwako, ya kwamba licha ya kukosa muda wa kukaa na kusoma kitabu, bado unaweza kujifunza kila siku, tena kwa muda w akutosha tu. Na habari hii njema ni kuhusu kujiunga na CHUO KIKUU KINACHOTEMBEA, yaani ulipo na chuo chako kipi.
Chuo kikuu kinachotembea ni nini?
Kama unakaa maeneo ya mijini, na nina hakika wengi hapa tunakaa maeneo hayo, usafiri kwenda kwenye shughuli zako mbalimbali ni kitu ambacho unafanya kila siku, au karibu kila siku. Mimi binafsi natumia muda usiopungua masaa mawili kwenye usafiri, kila siku, hasa siku za wiki. Asubuhi naendesha gari kwa muda usiopungua saa moja, na jioni naendesha muda usiopungua saa moja. Na siku nyingine uwepo wa foleni ndefu naweza kukaa barabarani hata masaa mawili au matatu kwa safari moja tu ya kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.
Huu ni muda ambao ungeweza kuwa unapotea bila ya kufanya chochote, au kama ukiamua kuutumia Kitanzania basi utaishia kumlaumu kila unayeweza kumlaumu kuhusu uwepo wa foleni ndefu. Lakini hilo halitakusaidia kwa sababu bado utaendelea kuwa kwenye foleni, na sio siku hiyo tu, na kesho yake tena na tena.
Badala ya kulalamikia muda unaopoteza kwenye foleni wakati unatoka sehemu moja kwenda nyingine, iwe kwenye usafiri wako binafsi au usafiri wa umma, unaweza kugeuza muda huu kuwa muda wa kujifunza. Na hapa ndio dhana ya CHUO KIKUU KINACHOTEMBEA inapokuja.


 
Unajifunzaje wakati upo kwenye usafiri?
Kushika kitabu na kuanza kusoma inaweza isiwe rahisi sana, hasa kama wewe ndio unaendesha usafiri binafsi, au umepanda kwenye usafiri wa umma ambao umejaza watu wengi na huenda wewe mwenyewe umesimama. Hivyo njia bora kabisa ya kujifunza katika hali hizi ni kusikiliza vitabu vilivyo somwa, kwa kiingereza vinajulikana kama AUDIO BOOKS.
Audio books hivi ni vitabu ambavyo vimesomwa na unachofanya wewe ni kusikiliza tu. Uzuri wa Audio books ni kwamba unaweza kusikiliza popote pale ulipo, kama unaendesha unaweka kwenye redio yako ya gari, kama upo kwenye daladala unaweka kwenye simu yako na unasikiliza kwa spika za masikioni, kama upo nyumbani unaweza kuweka kwenye redio au kompyuta na kama unafanya mazoezi unaweza kuweka kwenye kitu cha kusikilizia masikioni. Uzuri ni kwamba unaendelea na kile unachofanya na huku ukiendelea kupata maarifa mbalimbali ya kufanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Kwa mtu ambaye unaenda kwenye shughuli zako za kila siku kwa usafiri, kama ukijiwekea utaratibu wa kusikiliza kila siku, utashangaa baada ya muda mtazamo wako unabadilika kabisa. Utashangaa unaanza kuziona fursa zaidi, unapata hamasa ya kuweka juhudi zaidi kwenye kile unachofanya. Na pia utaanza kupata maarifa zaidi ya kufanikiwa kwenye kazi au biashara. Haya yatategemea na vitabu gani unasikiliza katika muda wako.
Na ili kujijengea tabia nzuri ya kujifunza kwa kusikiliza vitabu, jiwekee utaratibu kwamba unapopata dakika zaidi ya kumi za kusubiri kitu, basi sikiliza kitabu, na unapoingia kwenye chombo cha usafiri iwe binafsi au cha umma, sikiliza kitabu. Mimi nimejiwekea utaratibu nikiwasha tu gari basi kitabu kinaendelea kusomwa. Kwa njia hii sisikilizi kitu kingine kwenye gari zaidi ya vitabu.
Karibu upate AUDIO BOOKS.
Ili kuhakikisha unapata nafasi ya kujifunza popote unapokuwa, AMKA CONSULTANTS tunakupa nafasi ya kupata AUDIO BOOKS. Vitabu hivi vipo kwenye MEMORY CARD ya ukubwa wa 4 GB. Kadi hii unaweza kuiweka kwenye simu yako ya mkononi na kusikiliz akwa spika za masikioni, (ear phone) unaweza kuweka kwenye redio yako ya gari, na unaweza kuweka kwenye kifaa chochote kinachokubali kucheza muziki wowote.
Hivi sasa kuna memory kadi tatu na zina vitabu tofauti, vizuri sana kwako kujifunza na kujihamasisha ili kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Vitabu hivi kama ukivisikiliza naweza kukuahidi vitabadili sana maisha yako. Nina uhakika huo kwa sababu mimi ni mfano unaoishi wa manufaa haya.
MEMORY CARD YA KWANZA(MK1) 
Memory card hii inajumuisha vitabu hamsini ambavyo vimegawanyika katika makundi mawili.
Kundi la kwanza lina vitabu vifuatavyo;
  1. Cashflow quadrant – R. Kiyosaki
     2. Rich dad poor dad – R. Kiyosaki
     3. Increase your financial IQ – R. Kiyosaki
     4. Freedom or security – R. Kiyosaki
     5. Retire Young Retire Rich – R. Kiyosaki
     6. Brian Tracy – Become an Outstanding Manager
     7. Brian Tracy – 21 Success Secrets of Self-Made Millionaires
     8. Brian Tracy – Get Paid More and Promoted Faster
     9. Brian Tracy – How To Gain 2 Extra Hours a Day 
     10. Brian Tracy – 21 Ways to Build a High Profit Business
     11. Brian Tracy – 21 Ways To Get Ahead In Your Career
     12. Brian Tracy – Make a Million
     13. Brian Tracy – The Psychology of Achievement
     14. How To Instantly Connect With Anyone
     15. Napoleon Hill’s Keys To Success
     16. Anthony Robbins – Awaken the Giant Within
     17. Brian Tracy – 21 Great Ways To Manage Your Time And   Double Your Productivity
     18. Zig Ziglar – How To Be A Winner
     19. Zig Ziglar – Success And The Self-Image
     20. Earl Nightingale – Lead The Field
     21. James Allen – As A Man Thinketh
     22. Kerry L. Johnson – Science of Self Discipline
     23. David Lieberman – Get Anyone To Do Anything
     24. Eric Ries – The Lean Startup
     25. Outside Your Comfort Zone – Jeff Lilley
Kundi la pili lina vitabu vifuatavyo;
    1. 100 Ways To Motivate Yourself Change Your Life Forever – Steve Chandler
     2. Anthony Robbins – Lessons in Mastery
     3. Brian Tracy – Eat That Frog
     4. Carol Dweck – Mindset, The New Psychology of Success
     5. Dennis Waitley – Psychology of Winning
     6. Earl Nightingale – Great Ideas
     7. George S. Clason – The richest Man in Babylon
     8. Jim Rohn – Attracting Success
     9. Jim Rohn – Lessons in Leadership
     10. Kerry L. Johnson – Science of Self Discipline
     11. Robert Greene – 48 Laws Of Power
     12. Ross Jeffries – Unstoppable Confidence
     13. THE DIP, A Little Book That Teaches You When to Quit (and When to Stick)
     14. Unlimited Power  The New Science Of Personal Achievement
     15. Zig Ziglar – Goals
     16. 25 Ways to Win with People – John C Maxwell
     17. Becoming a Person of Influence – John C Maxwell
     18. Jim Rohn-Designing your life rather than making a living
     19. Og Mandino-Secrets to Success
     20. Robert Kreigel-If it aint broke–break it!
     21. The 21 Indispensable Qualities of a Leader Unabridged – John C Maxwell
     22. The Success Journey – John C Maxwell
     23. The Winning Attitude – John C Maxwell
     24. Tony Robbins-the decision that ensures your success
     25. We Are All Weird- The Myth of Mass and the End of Compliance
Memory kadi hii bei yake ni tsh elfu thelathini(30,000/=) . 
Kuipata kadi hii tuma fedha tsh elfu thelathini kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA 0717 396 253 kisha utapewa au kutumiwa kadi yako.
Kwa wale wa mikoani kadi itatumwa kwa basi hivyo unatakiwa kutuma fedha ya kadi na fedha ya nauli. Nauli ni tsh elfu kumi (10,000/=) hivyo jumla inakuwa tsh elfuarobaini(40,000/=), kadi pamoja na usafiri.
Tumia nafasi hii ya kipekee kuboresha maisha yako, kazi zako, biashara zako na hata ufanisi wako.

MEMORY CARD YA PILI(MK2) 
Memory card hii inakupatia elimu katika maeneo matatu muhimu sana.
Eneo la kwanza ni jinsi ya kuuza(sales), hiki ni kitu muhimu sana kwa kila mtu kujifunza kwa sababu kila mmoja wetu kuna kitu anauza.
Eneo la pili ni mbinu za mawasiliano(communication skills), mawasiliano yako ndio yatakupatia chochote unachotaka kwenye maisha yako, yafanye kuwa bora.
Eneo la tatu ni mbinu za kukubaliana(negotiation) katika maisha ya kila siku kuna vitu vingi ambavyo unahitaji kuwashawishi wengine ili wakubaliane na wewe, utajifunza kwenye kadi hii.
Memory Kadi hii ina ukubwa wa 4GB na ina vitabu 21.
VITABU VILIVYOPO KWENYE MEMORY CARD YA 2
1. Brian Tracy – Become a Sales Superstar
2. Brian Tracy – Effective Manager Series – Marketing
3. Brian Tracy – Psychology Of Selling
4. Effective and persuasive communication – Steven K. Scott
5. Jim Rohn – Building Your Network Marketing Business
6. Made for Success – Persuasive Selling and Power Negotiation
7. Magnetic Marketing [Tony Robbins, T Harv Eker, Robert Kiyosaki, Bob Proctor]
8. Personal MBA Business Crash Course
9. Robert Kiyosaki – Sales dogs 3 CDs
10. SalesBible
11. The Greatest Salesman in The World – Og Mandino
12. Think and Grow Rich
13. Tom Hopkins & Laura Laaman – The Certifiable Salesperson
14. Unlimited Selling Power by NLP
15. Zig Ziglar – Secrets of Closing the Sale
16. Zig Ziglar – Sell Your Way To The Top
17. Becoming a Person of Influence – John C Maxwell
18. Running With the Giants Unabridged – John C Maxwell
19. Tom Hopkins-Avoiding the 10 biggest sales and marketing mistakes
20. Zig Ziglar – keys to closing
21. Zig Ziglar-Today-the first day of the rest of your life

Jinsi ya kupata memory kadi hii.
Memory kadi hii yenye vitabu hivi gharama yake ni tsh 30,000/=. Kama upo dar es salaam utapatiwa kadi yako na kama uko mkoani utaongeza tsh 10,000/= kwa ajili ya usafiri na utatumiwa kadi yako huko uliko. Kuipata kadi hii tuma fedha tsh elfu thelathini kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA 0717 396 253 kisha utapewa au kutumiwa kadi yako. Wahi nafasi hii ya kipekee ya kuongeza ujuzi wako ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.
MEMORY CARD YA TATU(MK3)
VITABU VILIVYOPO KWENYE AUDIO BOOKS CARD 3
1. The 7 Habits Of Highly Effective People – Steven Convey
Hapa utajifunza tabia saba za watu wenye ushawishi mkubwa na mafanikio pia. Unataka kufikia mafanikio makubwa? Fanyia kazi tabia hizi saba.
2. Donald Trump – Never Give Up
Katika kitabu hiki bilionea mwekezaji kwenye majengo Donald Trump anatushirikisha mbinu alizotumia yeye kutoka kwenye madeni mpaka kufikia kuwa bilionea kwa kuwekeza kwenye majengo, tena bila hata ya kuanza na fedha zake mwenyewe. Sikiliza kitabu hiki.
3. Anthony Robbins – Time of Your Life
Ningekuw ana muda ningefanya hiki, ningefanya kile na kadhalika. Hizi ni kauli maarufu sana kwa watu wengi. Anthony Robbins anakuambia una muda mwingi kuliko unavyofikiri. Muda huo uko wapi? Pata memory card na usikilize kitabu hiko.
4. Your Right To Be Rich – Napoleon Hill
Unafikiri wewe huna haki ya kuwa tajiri? Unakosea sana, haki yako ipo, sema hujaijua ili uweze kuidai na kuisimamia. Napoleon Hill anakupa haki yako kwenye kitabu hiki.
5. Rich Dad’s Guide to Investing – Robert Kiyosaki
Kama mpaka sasa hujaanza kuwekeza, upo kwenye hatari kubwa. Kama utapita siku ya leo bila ya kujifunza kitu kuhusu uwekezaji na kukifanyia kazi, hakuna kitakachokusaidia kwenye dunia hii. Robert Kiyosaki anakupatia muongozo mzuri sana wa uwekezaji kwenye kitabu hiki, ni wewe kusikiliza tu.
6. Guide to Becoming Rich – Robert Kiyosaki
Robert kiyosaki na hapa tena anaendelea kukupa mbinu nzuri za kuweza kufikia utajiri. Haihitaji uibe au udhulumu, haihitaji uende kwa mganga, bali inahitaji wewe kujua misingi na kuifuata, na utajiri unakuja wenyewe.
7. 177 Mental Toughness Secrets of the World Class – Steve Siebold
Kuna tofauti kubwa sana ya kimawazo kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa. Steve Siebold anakupa siri 177 za watu waliofanikiwa sana ambazo watu wasiofanikiwa hawazijui. Unataka kuzijua? Pata kadi hii na sikiliza hiko kitabu.
8. Lessons from the Richest Man Who Ever Lived – Steven K. Scott
Kitabu hiki kina masomo muhimu sana kuhusu maisha na mafanikio kutoka kwa mtu tajiri sana aliyewahi kuishi na pia mtu mwenye busara sana kuwahi kutokea. Huyu ni mfalme Selemani. Steven Scott amekuchambulia siri muhimu za maisha kutoka kwenye maandiko ya Mfalme Selemani, nakusihi sana, usiache kusikiliza kitabu hiki. Yaani ni tuisheni kamili ya maisha, sio mafanikio na utajiri tu.
9. Neil Cavuto – Your Money Or Your Life
Maisha ni kuchagua na kila unachochagua kila siku kinakupeleka kwenye umasikini au kwenye utajiri. Sikiliza kitabu hiki ufanye maamuzi yatakayokupeleka kwenye utajiri.
10. Anthony Robbins – Power To Influence
Mafanikio yako kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla yatatokana na jinsi unavyoweza kushawishi wale watu ambao ni muhimu kwako. Utamshawishije mteja anunue? Utamshawishije boss akuongeze mshahara? Anthony Robbins anakupa mbinu hizo, utazisikiliza hapa.
11. Anthony Robbins – Personal Training System
Kutengeneza mkakati wa kubadili maisha yako sio kitu rahisi. Anthony anakupa mfumo mzuri utakaoweza kuutumia kujifunza na kubadili maisha yako. Utasikiliza na kujifunza hapa.
12. David Bach-The Automatic Millionaire
David Batch anakupa siri ambazo zitakuwezesha wewe kufikia utajiri hata kama unapata kipato cha kawaida. Anakupa siri ambayo watu wengi wameitumia kufikia utajiri kwa kufuata misingi mizuri na kwa muda mrefu. Kama hutaki misukosuko ya kibiashara, unapenda kuendelea na kazi ya kuajiriwa lakini pia ufikie utajiri basi sikiliza kitabu hiki.
Sina mengi ya kuongeza hapo, elimu kubwa sana ipo kwenye vitabu hivyo kumi na mbili, ni wewe kujipatia kadi yako na kila siku kusikiliza vitabu hivyo.
Kadi inapatikana kwa gharama ya tsh elfu thelathini(30,000/=), na kama upo mkoani utaongeza fedha ya nauli na utatumiwa ulipo. Nauli inakuwa tsh elfu kumi(10,000/=).
Kupata kadi hii tuma fedha kwenye namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha utaandaliwa kadi na kupewa au kutumiwa. Kama upo dar tuma tsh elfu 30, kama mkoani tuma tsh elfu 40. Tuma fedha na maelezo kisha utapatiwa kadi yako.
Kujifunza kila siku ndio msingi wa mafanikio.
JIFUNZE, JIFUNZE, JIFUNZE.

MUHIMU;
Audio Books hizi zinatolewa kuanzia leo jumatatu tarehe 15/02/2016 mpaka ijumaa tarehe 19/02/2016. Hivyo kama hutaki kukosa nafasi hii ya kipekee, tuma fedha kama maelezo yalivyo hapo juu kisha tuma ujumbe unahitaji KADI NAMBA NGAPI yaani kama ni MK1 MK2 au MK3. Kisha utafanyika utaratibu wa kukupatia kadi hiyo kulingana na ulipo.
Karibu sana na tumia nafasi hii ya kujifunza ili kuboresha maisha yako zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: