Hongera rafiki yangu kww nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweks juhudi zaidi kwenye kile tulichochagua kufanya ilo tuweze kupata matokeo bora zaidi.
Rafiki, tutumie muda wa leo vizuri, maana ukishapita hatuwezi kuupata tena kwenye maisha yetu.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu STATUS QUO…..
Kikwazo kimoja cha mafanikio kwenye maisha yetu, ni kufanya mambo kwa mazoea. Ukishajikuta unafanya kitu kwa sababu jana na juzi ulifanya hivyo, tayari umeanza kupotea.
Sumu nyingine kubwa kabisa ya mafanikio ni kufanya vitu kwa sababu ndiyo hivyo tunafanyaga, hii ndiyo status quo kwenye ubora wake. Yaani unafanya kitu siyo kwa sababu kina umuhimu, ila kwa sababu ndivyo ambavyo huwa tunafanya.
Unachukua hatua fulani kwa sababu ndiyo hatua ambayo watu wanachukuaga wakiwa kwenye hali kama hiyo.
Kuishi maisha ya STATUS QUO ni kujidharau na kusahau uwezo mkubwa uliopo ndaninyako.
Unapoanza kufanya mambo kwa sababu kila mtu anafanya, hapo ndipo unapoweka uwezo na utofauti wako pambeni. Unaacha kuwa wewe na unakubali kuwa kama kila mtu mwingine.
Ubaya wa kuwa kama kila mtu mwingine ni kwamba hakuna kitakachowavuta watu kuja kwako.

Status quo inaharibu uwezo na kuwafanya watu kushindwa kufanikiwa.
Asubuhi ya leo hebu zifunue status quo zote kwenye maisha yako. Angalia namna unaendesha maisha yako na jiulize kwa nini unafanya kila unachofanya? Una sababu bora kwako au unafanya kwa sababu kila mtu anafanya? Au ndivyo ilivyozoeleka kufanya?
Ondoa status quo zote kwenye maisha yako. Ishi maisha yenye maana kwako.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info