Taarifa Muhimu Kuhusu Semina Ya Milioni Ya Ziada Kwa Wale Ambao Walishindwa Kushiriki


Rafiki,
Tarehe 30/10/2016 tulifanya semina kubwa ya MILIONI YA ZIADA ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar. Ilikuwa ni semina kubwa ambapo washiriki walijifunza mambo mengi na hatua zakuchukua ili kushika hatamu ya maisha yao hasa kwenye upande wa fedha.
Wakati tunatangaza semina hii, kulikuwa na maombi mengi kutoka kwa watu wa mikoani ambao walipenda sana kushiriki semina hii. Tuliwasihi wengi wajipange kusafiri ili wasikose semina hii, wengi sana walisafiri kutoka mikoa mbalimbali. Lakini wapo ambao walishindwa kabisa kusafiri kutokana na majukumu mbalimbali. Wapo ambao walipenda sana kushiriki semina hii lakini walikosa ruhusa kwenye maeneo yao ya kazi.
Watu hawa waliomba sana tutafute njia ili na wao wapate mafunzo ya semina hii. Wengi waliomba turekodi mafunzo ya semina hii kwa mfumo wa cd au dvd na wanunue. Hili halikuwezekana, kwa sababu ni mchakato mwingine ambao hatukuwa na maandalizi nao na lengo la semina yetu lisingeweza kufikiwa kwa njia ya cd au dvd. 
Tulichotaka ni kuwa na kitu ambacho ni live, mtu ahudhurie, kuna nguvu kubwa sana ya kuwa kwenye semina, au kufuatilia semina moja kwa moja tofauti na ukiangalia dvd.
Baada ya kufikiri kwa kina, tulipata wazo la kuandaa WEBINAR, ambapo tungeendesha semina kama hiyo kwa njia ya mtandao. Kwa namna hii semina ingekuwa live, lakini unaweza kuifuatilia popote ulipo, ukiwa na mtandao wa intaneti. Pia ungeweza kuuliza swali moja kwa moja wakati semina inaendelea na ukapata majibu ya swali lako.
Baada ya kupata wazo hili tuliahidi kwamba wale watakaokosa semina hii, basi wataweza kushiriki kwa njia ya mtandao. Lakini kipaumbele cha kwanza ilikuwa ni kuhudhuria, na kama ukishindwa kabisa basi utaweza kupata kwa njia ya mtandao.
Leo kwa masikitiko makubwa napenda kusema ya kwamba hatutaweza kuendesha semina tuliyoahidi kuendesha kwa njia ya mtandao yaani WEBINAR. Nasema hili kwa masikitiko makubwa kwa sababu napenda kutimiza kile ambacho ninawaahidi watu, naumia sana pale ambapo navunja ahadi zangu mwenyewe. Lakini unafika wakati unakuwa huna namna bali kuvunja.
Kwa nini hatutaweza kuendesha semina hii ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao?
Ipo sababu kubwa moja ambayo ni tatizo la nchi yetu kwenye mtandao wa intaneti. Ili kuendesha semina moja kwa moja kwa njia ya mtandao, wafuatiliaji wa semina hiyo wanapaswa kuwa na mtandao imara. Mtandao wenye nguvu ya kuweza kufuatilia video inayorushwa kwenye mtandao wakati huo huo. Kwa sababu kwenye webinar, tunachofanya ni kurekodi video na wakati huo huo inarushwa kwenye mtandao na wewe unaifuatilia. Sasa watu wengi hawana mtandao imara, hivyo ni vigumu kuweza kufuatilia moja kwa moja bila ya kukatika katika. Watu wengi waliopo mikoani hawana mtandao wa uhakika kuweza kufuatilia video kwa zaidi ya saa moja kupitia mtandao wa intaneti bila ya kukatika.
Tatizo jingine kubwa ni kwamba wasomaji wetu wengi wanatumia vifaa vya mkononi kufuatilia masomo yetu, wengi mno wanatumia simu. Kufuatilia webinar kwa simu ni ngumu mno, unahitaji kompyuta ambayo ina mtandao mzuri wa intaneti ili uweze kufuatilia webinar vizuri.
Kwa majaribio ambayo tumeshafanya mpaka sasa kwa webinar, tunaona wengi wanashindwa kupata mtiririko wa moja kwa moja. Hivyo kama tungekuambia ulipe fedha ya semina halafu tunaenda hewani na wewe ukawa hutupati, ingebidi tuache kuendesha semina na kuhakikisha unatupata, sasa hebu fikiria hivyo wa watu 100 wengine ambao wangekuwa na changamoto kama hiyo. Kwa hiyo hili lingeleta usumbufu kwa kila mmoja wetu.
Hivyo tumeona ya kwamba hatutaweza kuendesha semina hii kwa njia ya mtandao. Badala yake kila mwaka tutafanya semina moja kubwa ya aina hii, na semina hiyo itakuwa ni ya kuhudhuria pekee. Hakutakuwa na cd wala dvd, utahitaji kuhudhuria moja kwa moja ili kuweza kujifunza. Taarifa tutakuwa tunatoa mapema ili uweze kujipanga kama ni kusafiri ili uweze kufuatilia mafunzo ya semina hizi. Hatuwezi kuahidi kupata mafunzo ya semina hizi kwa njia nyingine yoyote zaidi ya kuhudhuria moja kwa moja.
Nirudie tena kuomba radhi kwa usumbufu huu. Najua wengi mlikuwa mnasubiri semina hii kwa hamu na shauku kubwa kwa sababu mara nyingi mmekuwa mnaniuliza semina niliyoahidi ni lini. Najua wengi mmeumia kwa hili, na naelewa kabisa, lakini kwa upande wetu hatuna namna bora ya kulifanya hili kwa sasa.
Semina nyingine kwa njia ya mtandao zitaendelea kukujia, semina ya kuanza mwaka 2017 na kuufanya kuwa mwaka wa mafanikio makubwa itaanza tarehe 02/01/2017. 
Itaenda kwa siku kumi, nitakushirikisha yale tutakayojifunza kwenye semina hii siku chache zijazo. Semina hii itaendeshwa kwa njia ya wasap peke yake. Taarifa zaidi nitakuletea rafiki. Pia mwaka 2017 yapo mengi makubwa sana ninayokuandalia rafiki, lengo ni wewe uwe na maarifa sahihi yatakayokuwezesha kufanya maamuzi bora ili kuwa na maisha ya mafanikio.
Najaribu kufanya kila lililopo ndani ya uwezo wangu, kuhakikisha maarifa yote niliyonayo na ninayoendelea kuyapata na wewe rafiki yangu unayapata pia. Kwa sababu kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kwamba maarifa sahihi yanaleta fikra sahihi na fikra sahihi zinatengeneza matendo sahihi na bora.
Natumaini tutaendelea kuwa pamoja rafiki yangu, kama utakuwa umekerwa kiasi cha kushindwa kuendelea kuwa pamoja, pia naelewa hilo, na sitakulaumu kwa hatua yoyote utakayoamua kuchukua, iwe ni kuacha kusoma kabisa, au kuacha kuhudhuria semina nyingine ninazotoa. Fanya kile ambacho ni sahihi kwako, kwa sababu maarifa ninayotoa ni kwa ajili yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: