Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

IMG_20170102_073855
Tutumie nafasi hii ya leo vizuri ili tuweze kupata matokeo bora.
Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana siku ya leo.

Asubuhi ya leo tutafakati kuhusu TOILET (CHOO) NA TEMPLE (HEKALU).
Choo kinaingia kila kitu, hakichagui, kila uchafu unaingia chooni. Na hata kama siyo uchafu, ukiwekwa chooni unaenda tu, kwa sababu choo hakina kuchagua, kila kitu kinaingia.

Kila kitu hakiwezi kuingia hekaluni, hekalu linachagua, uchafu hauingii hekaluni. Hekalu ni mahali pasafi ambapo kilicho safi ndiyo kinaingia. Uchafu hauna nafasi kwenye hekalu.

Swali ni je, mwili wako unauchukulia kama hekalu au kama choo?
Je akili yako unaichukulia kama hekalu au kama choo.

Wengi wanaruhusu kila kitu kiingie kwenye miili yao,
Vyakula vya ajabu ajabu,
Pombe za kila aina,
Sigara.
Madawa ya kulevya,
Na uchafu wa kila aina ambao unaweza kupatikana.

Na hata akili zao, wanaruhusu kila uchafu uingie,
Habari hasi,
Habari za udaku,
Umbea umbea,
Na mengine kama hayo.

Tatizo la choo ni kwamba, uchafu unaingia na uchafu unatoka, yaani kinachotoka chooni nacho ni uchafu.
Hivyo kama unaruhusu mwili na akili yako viwe choo, utakachokuwa unatoa ni uchafu.
Akili ikiwa na uchafu, unachoongea ni uchafu.

Hekalu ni safi na linatoa usafi.
Ufanye mwili wako na akili yako kuwa hekalu,
Ruhusu usafi pekee ndiyo uingie kwenye mwili na akili yako.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki,
Epuka kufanya mwili na akili yako kuwa choo, chagua sana kipi unaruhusu kiingine.
Leo hii nenda KATHUBUTU, USHINDE na USHUKURU.

Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.