USHAURI; Kwa Nini Ukipata Fedha Nyingi Haikai Na Wala Hutulii.

Kila mtu anajua ni kwa namna gani fedha ilivyo muhimu kwenye maisha yetu, ni muhimu sana kwa sababu vitu vyote muhimu kwenye maisha tunavipata kwa fedha. Na hii ndiyo imepelekea sisi binadamu kutumia muda wetu mwingi kwenye kutafuta fedha, ili tuweze kupata yale muhimu sana kwenye maisha.

Lakini kwenye swala la fedha, tuna changamoto kuu moja, hatuna elimu ya kutosha kuhusu matumizi na usimamizi wa fedha binafsi. Kitu ambacho tunaweza kuwa tumefundishwa au kujifunza wenyewe kupitia wengine ni namna ya kupata fedha. Ndiyo maana kila mtu ana shughuli fulani anayoifanya ambayo inamwingizia kipato.

Kasheshe inaanzia pale mtu anapopata hizo fedha, wapo ambao wanazitumia vizuri na kufanikiwa sana, na wapo ambao wanashindwa kuzitumia vizuri na kuishia kuwa masikini. Ni katika matumizi ya fedha ndipo wanapozaliwa matajiri na masikini. Ndipo tofauti kuu inapoanzia.

Kumekuwa na malalamiko mengi ya watu juu ya fedha kutokukaa. Wengi wanasema wakipata fedha, hasa ambayo ni nyingi kuliko walivyozoea, imekuwa haikai. Watu wanapopata fedha hiyo nyingi wanasahau kabisa mipango waliyowahi kuwa nayo huko nyuma, wanajikuta wakifanya mambo ya ajabu mpaka fedha zile zinapokwisha. Fedha zikiisha tu, akili zinarudi vizuri na kuanza kujutia nini wamefanya.

Tumekuwa tunaona watu wengi wanaopata fedha nyingi kwa pamoja wanakoishia. Angalia watu wanaostaafu na kupokea mafao yao, unashangaa wakifanya mambo ya ajabu mpaka fedha ile inaisha. Au watu walioshinda bahati nasibu ya fedha nyingi, baada ya muda wanaishia kuwa masikini kabisa. Wapo pia wanaochimba madini, wanapopata madini ya thamani, wengi hawajui zile fedha zinakwenda wapi.

Kumekuwepo na dhana nyingi kwenye jamii juu ya hali hii. Wengine wamekuwa wanasema kuna watu wanatumia nguvu za uchawi katika kuwachukulia wengine fedha. Wengine wanasema wapo chuma ulete ambao wanavuta fedha za watu. Lakini rafiki yangu mimi nataka nikuambie ukweli, na siku zote ukweli siyo mtamu.

Siyo kweli kwamba kuna namna ya ajabu fedha hizi zinachukuliwa, bali mtu mwenyewe anachagua kupoteza fedha zile nyingi kwa sababu kubwa ya kisaikolojia ambayo nakwenda kukushirikisha leo.

Kila mtu ana kiwango chake cha fedha kwenye mawazo yake. Hichi ni kiwango ambacho lazima awe nacho ndiyo maisha yake yatulie, ikizidi hapo atajikuta anafanya mambo ya ajabu mpaka arudi kwenye kile kiwango, na ikipungua pia atapambana sana mpaka apate fedha za kumtosheleza. Ni hali hii ndiyo imepelekea wengi kupoteza fedha wanapozipata nyingi kwa wakati mmoja.

Angalia kipindi hichi cha leo, nimeeleza hilo kwa kina, na namna unavyoweza kuishinda hali hiyo ili hata ukipata bilioni moja leo, uweze kutulia na kufanya mambo makubwa.

Angalia kipindi hicho hapo chini na kama hukioni basi bonyeza maandishi haya kuangalia kipindi.

 

Nina imani yapo makubwa uliyojifunza kupitia kipindi hichi cha ONGEA NA KOCHA. Karibu sana tuendelee kuwa pamoja na kama kuna swali lolote ungependa nijibu, au kitu chochote ungependa nikushauri, weka maoni chini ya kipindi hicho ulichoangalia.


Nakutakia utekelezaji mwema wa yale uliyojifunza.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: