Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002
Tutumie nafasi hii ya leo vizuri ili tuweze kufanya makubwa.
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana siku hii ya leo.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kinachotusukuma.
Chochote tunachofanya, ni kwa sababu tuna msukumo ndani yetu.
Bila ya msukumo ni vigumu kufanya chochote, na uvivu mara nyingi unatokana na kukosa msukumo.

Sasa kile tunachofanya, namna tunavyokifanya na hata matokeo tunayopata, inategemea sana aina ya msukumo tulionao.

Upo msukumo wa HOFU YA KUKOSA AU KUSHINDWA. Hapa mtu unafanya kwa sababu unahofia usipofanya utashindwa, na mambo yatakuwa hovyo kwako. Unafanya kwa hofu kubwa, na hivyo hufurahii kile unachofanya.
Unafanya kwa kile kiwango ambacho kitakuzuia wewe kushidwa, zaidi ya hapo hakuna.

Pia upo msukumo wa HAMASA YA KUPATA AU KUSHINDA. Hapa unafanya kwa sababu unajua unachokipata kitakuwa bora sana, utakuwanna ushindi na maisha yako yatakuwa bora sana.
Kwa hamasa hii unaweka juhudi kubwa, unafanya makubwa na unakwenda mbali kuliko ulivyotegemewa kwenda.

Swali ni je, kazi unayofanya sasa, biashara unayofanya na hata maisha unayoishi, nini kinakusukuma? Je ni hofu ya kukosa au hamasa ya kupata.

Wanaofanikiwa ni wale wanaosukumwa na hamasa ya kupata, na wanapata makubwa.
Wanaosukumwa na hofu ya kukosa wanaishia kutokukosa, lakini hawapati makubwa.
Wewe unaelekea kupata nini?
Jua hamasa uliyonayo sasa na tengeneza iliyo bora zaidi.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.