Hongera rafiki yangu kwa siku hii ya kipekee sana ya leo.
Ni siku ambayo hutaiona tena kwenye maisha yako, ni leo tu hivyo ni muhimu uitumie vizuri siku hii.

img-20161217-wa0002
Tukumbuke msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao unatuwezesha kufanya makubwa kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu ku TAKE ACTION OR MOVE ON…
Kuna mambo mengi ambayo haturidhishwi nayo kwenye maisha,
Na hivyo kutaka kupata kilicho bora zaidi.
Sasa wengi wamekuwa wakilalamikia tu kile wanachopata au walichokosa na kuishia hapo.
Hiyo ni kwa sababu kulalamika pekee ni rahisi.
Lakini malalamiko ya kuongea tu, hasa kuongelea pembeni hayajawahi kumsaidia mtu.
Muhimu ni ku TAKE ACTION, kuchukua hatua kwa lile ambalo halijaka sawa. Mfuate anayehusika na mweleze wazi, au kile ambacho hakijakaa sawa kiweke sawa.
Na endapo basi hayo hayawezekani, basi kuendelea kulalamika ni kupoteza muda wako. Ni bora uka MOVE ON, SONGA MBELE NA MAISHA YAKO.
Kwa sababu unapoendelea kulalamikia kitu ambacho huwezi kuchukua hatua, unachofanya ni kupoteza tu maisha yako, na kuwachosha wale wanaokusikiliza.
Unaweza kuwa mzigo mpaka watu wanaamua kukukimbia, wakikuona wanajua wa kulalamika amekuja.
Hivyo rafiki kumbuka hili, TAKE ACTION OR MOVE ON.
Haya maisha ni mazuri sana kama ukishaelewa unachotaka, usipoteze muda wako kwa mambo ambayo hayana matokeo yoyote kwako.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.