Habari rafiki yangu?

Karibu tena kwenye somo letu la leo la video za ONGEA NA COACH ambapo tunashirikishana mambo muhimu sana kwa ajili ya mafanikio yetu. Nimekuwa na msimamo mmoja mkuu kuhusu maisha yangu na hata yako rafiki yangu. Msimamo huo ni kwamba MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA, hakuna anayeweza kukuzuia, wala hakuna atakayekupa kama wewe mwenyewe hutoamua kufanikiwa. Na hapa namaanisha mafanikio kwenye kila eneo la maisha yako.

UTAJIRI VS UMASIKINI.

Moja ya eneo ambalo watu wengi wamekuwa wakipotea ni kwenye kuutafuta utajiri. Kwa sababu wengi hufikiri utajiri ni jinsi unavyoweza kulipwa fedha nyingi kwa kazi au biashara ambayo unaifanya. Ndiyo maana wengi hukazana kufanya kazi masaa mengi zaidi, kuongeza utaalamu zaidi kwa matarajio kwamba kipato kitakuwa zaidi.

Lakini mimi nimekua nakuambia hivi; UMASIKINI NI PALE UNAPOIFANYIA KAZI FEDHA, NA UTAJIRI NI PALE FEDHA INAPOKUFANYIA KAZI WEWE. Hapa nina maana kwamba, kama kipato chako ni cha moja kwa moja, yaani ili upate fedha lazima ufanye kazi wewe mwenyewe, basi bado upo kwenye umasikini, haijalishi unapata kipato kikubwa kiasi gani. Hii ni kwa sababu kutegemea kipato cha moja kwa moja, siku kinapokatika, na mara nyingi hukatika, unajikuta kwenye wakati mgumu.

Ili ufikie uhuru wa kifedha, ili uwe tajiri, unahitaji kuifanya fedha yako ikufanyie wewe kazi. Na moja ya njia za kuifanya fedha ikufanyie wewe kazi ni kuwekeza. Maana unapowekeza, fedha yako inafanya kazi bila ya wewe kuwepo moja kwa moja.

Yapo maeneo mengi ya kuwekeza, na moja muhimu ni kuwekeza kwenye hisa. Uwekezaji kwenye soko la hisa ni kitu ambacho ni kigeni kwa wengi, wengi hawaelewi na wamekuwa wanafikiri ni kitu kigumu kinachohitaji akili nyingi na elimu kubwa.

Leo nimekuandalia somo muhimu kuhusu uwekezaji kwenye somo la hisa. Katika somo hili nimekueleza maana ya hisa ni nini, kwa maneno rahisi kabisa utakayoelewa. Nimekupa na mfano ambao utakufanya uelewe sana.

Pia nimekupa faida na hasara za kuwekeza kwenye soko la hisa na kwa nini uwekeze licha ya kuwepo kwa hasara.

Mwisho nimekushirikisha fursa ya uwekezaji kupitia hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania. Hizi ni hisa ambazo zimeingia kwenye soko la awali kuanzia tarehe 09/03/2017 mpaka tarehe 19/04/2017. Nimekueleza faida na hasara za hisa za vodacom na pia nimekueleza kwa nini uzinunue.

Hili ni somo ambalo hupaswi kwa namna yoyote ile kulikosa, maana litakupa mwanga mkubwa sana.

Unaweza kuangalia somo hilo kwa kubonyeza maandishi haya.

Au kama kifaa chako kina uwezo wa kuonesha moja kwa moja, angalia hapo chini,

Kuangalia masomo ya nyuma, kuhusu siri za fedha na mafanikio, bonyeza maandishi haya.

Kusikiliza vipindi vyangu vingine vya sauti ambapo utajifunza mengi zaidi, bonyeza maandishi haya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.