Biashara yako ina wateja ambao ni wale watu wanaonunua kwako sasa. Hawa tayari wanakujua na wanajua ni kipi unachotoa na kinawasaidiaje.

Lakini pia biashara yako ina wateja watarajiwa. Hawa ni wale watu ambao bidhaa au huduma unayotoa inawafaa na itawasaidia, ila bado hawajawa wateja wako bado.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha wasiwe wateja wako mpaka sasa.
1. Huenda hawajui kama upo.

  1. Huenda wanapata huduma zinazowatosheleza walipo sasa.

  2. Huenda hakuna tofauti yoyote kwako na kule walipo sasa.

Kama mfanyabiashara, mara zote wafikirie wateja wako watarajiwa. Jua sababu zinazowazuia kuwa wateja wako na zifanyie kazi ili uweze kuwafikia na kuwapata wateja hawa.

Hakikisha unatoa huduma bora zaidi kila wakati na unajitofautisha na wafanyabiashara wengine.

Pia watumie wateja ulionao sasa kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi.

Kila la kheri kwenye biashara yako.