Kama hutaki mafanikio,

Hutaki maisha bora kabisa kwako,

Hutaki uhuru wa kipato na kuondokana na madeni.

Hutaki kuwa na afya bora na kuepukana na magonjwa,

Na pia hutaki kabisa kuwa na biashara au kazi yenye kipato kizuri,

Basi umepotea njia, hapa siyo sehemu yako, nitakukasirisha na kukukwaza kwa mambo ambayo hayakuhusu. Hivyo unaweza kuishia hapa na kuwaacha wale wanaotaka vitu hivyo wapate kile wanataka.

Karibu sasa kwa kuwa najua kabisa unataka mafanikio, unataka utajiri, unataka afya bora na maisha bora. Na mimi rafiki yako, nakwenda kuongea na wewe moja kwa moja, mubashara kabisa, bila ya kukuficha chochote.

Huenda unapambana sana kuhakikisha unapata kile unachotaka. Unakazana na kazi, hupumziki lakini bado unajikuta upo pale pale. Mpaka wakati mwingine unapata hisia labda kuna watu wamekufanyia mambo ya kishirikina usifanikiwe, au wale wanaofanikiwa kuna mambo wamefanyiwa yanawasaidia zaidi.

Sasa kabla hujaendelea kujidanganya na hayo rafiki yangu, nimekuletea somo ambalo litakufungua kabisa. Somo hili litakuonesha wapi ambapo unakosea na hivyo kushindwa kufika unakotaka kufika.

Kwa kuangalia somo hili la leo, na ukafanyia kazi, hutabaki hapo ulipo. Naweza kukuhakikishia hilo kwa sababu miaka michache iliyopita nilikuwa nafanya kosa kama unalofanya wewe, nilipogundua na kurekebisha, nimekuwa naona matokeo mazuri.

Nisikucheleweshe, nenda kwenye somo hili moja kwa moja kwa kubonyeza maandishi haya. Au unaweza kuliangalia hapo chini iwapo kifaa chako kinaruhusu.

Ninachokuambia ni hichi rafiki, jifunze, pata maarifa, fanyia kazi. Hivyo ndivyo maisha yanavyoboreshwa, kwa juhudi na siyo kwa bahati.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.