KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 61 – 70.
Socrates anatuasa kuuliza maswali bora ili kuweza kupata ukweli wa mambo na hata kujijua sisi wenyewe kwa kina.
Watu walioishi falsafa ya Socrates wamekuwa watu wa kuhoji wengine na kujihoji kwenye kila jambo ili kuweza kufikia ukweli.
Mwanasaikolojia Harry Dunne amekuwa akiwauliza watu swali moja muhimu wakati wa kuwashauri, ambalo linawafanya kujitafakari na kuona majibu wao katika kuboresha mahusiano yao.
Hasa kwenye mahusiano ya ndoa, ambapo kila mtu huwa anaona yupo sahihi, Dunne amekuwa akiwataka watu wajiulize swali moja tu;
Ingekuwaje kama wewe ungekuwa umeoa/umeolewa na wewe.
Yaani vipi kama wewe ndiyo yule mtu uliyemuoa au aliyekuoa?
Je kwa tabia na namna ulivyo, ungeweza kuvumilia kuishi na mtu kama wewe?
Kama ukiona kuna kitu usingekubaliana nacho basi unakibadili ili kuweza kuboresha mahusiano yenu.
Unaweza kujiuliza swali hili kwenye maeneo mengine muhimu ili kuwa bora zaidi.
Kwa mfano kama umeajiriwa, jiulize kama wewe ndiyo ungekuwa mwajiri, je ungemwajiri mtu mwenye tabia kama zako?
Kama upo kwenye biashara jiulize je kama wewe ungekuwa ndiyo mteja, je ungenunua kwa mfanyabiashara kama wewe?
Jiulize swali hili na chukua hatua, utakuwa bora zaidi.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa