The greatest remedy for anger is delay. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Leo ni fursa nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuyaendeleza mafanikio yetu ya jana na siku zilizopita.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Leo tuianze siku yetu kwa kutafakari DAWA YA HASIRA…
Ukitaka hasira zisikusumbue, zisikutawale na wala zisiwe kikwazo kwako kufanikiwa, basi dawa ni moja, kuwa na SUBIRA.
Kuwa mtu wa kusubiri badala ya kuchukua hatua haraka na hatua za hovyo, kutakuepusha na madhara mengi ya hasira.

Hata kama mtu amefanya kitu ambacho kinakukasirisha namna gani, kuwa na subira, subiri kidogo kabla hujachukua hatua yoyote.
Pale unapokuwa na msukumo ndani yako wa kujibu au kuchukua hatua, acha kwanza kuchukia hatua.
Jilazimishe kutulia na kupata udhibiti wa akiki yako, na hasira hazitakuwa kikwazo kwako.

Ukiweza kutulia, kuwa na subira, hasira zinayeyuka na hazitakuwa na madhara kwako. Lakini kama utakuwa mtu wa kuchukua hatua haraka kwa kila kinachokupa hasira, utakuwa mtumwa wa hasira.

Pale unapoona hasira zimekupanda na kukubana kiasi kwamba huwezi kutulia kabisa, jipe dakika chache za kupumua, ndiyo, kupumua pekee kunakutosha kuondoa sehemu kubwa ya hasira.

Ukiwa na subira, hasira hazina madhara kwako.
Uwe na siku njema sana leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa