Habari za leo rafiki?

Ni matumaini yangu kwamba upo vizuri na umeamka ukiwa na hamasa ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana kwenye maisha yako kwa siku ya leo.

Napenda kuchukua nafasi hii kukutaarifu ya kwamba, semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2017 ilikamilika kwa mafanikio makubwa sana. Semina hii ilifanyika tarehe 28/10/2017 dar es salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Golden Park Hotel.

Imekuwa ni semina iliyowaleta wanamafanikio wote kwa pamoja, wakafahamiana, kujifunza kwa pamoja na kujenga mtandao imara wa ushirikiano kwenye mambo mbalimbali.

Nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wanamafanikio na marafiki wote kwa ujumla kwa semina hii. Kwa wale waliohudhuria nawashukuru sana na kuwapa hongera, na wito wangu mkubwa kwetu sote ni kwenda kuyafanyia kazi yale ambayo tumejifunza kwenye semina hii. Twende tukabadili maisha yetu, tukaboreshe kila tunachofanya ili tuweze kupata matokeo tofauti kabisa.

Pia niwashukuru sana wale wote ambao hawakuweza kufika lakini tumekuwa pamoja kwenye kujifunza. Ni kwa ajili yenu wote mimi naendelea kufanya kazi hii. Hivyo kama hukufika usione kama nimekutenga au umepotea, bado tupo pamoja, tutaendelea kujifunza pamoha, na mwaka 2018 itakuwepo semina nyingine kama hii, hivyo unaweza kujipanga na kuhudhuria.

Kwenye semina walikuwepo watu walikuwa na wasiwasi wa kulipia ada ya kushiriki, wakiona labda watapoteza fedha au kuibiwa. Niliwaambia vyema wachague kulipia au waache mpaka mwaka kesho. Wapo ambao hawakuweza kuvumilia na kulipa, hawajajutia walichofanya.

Nitaambatanisha hapa baadhi ya picha za matukio ya semina hii ya kipekee ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama ulikosa semina ya mwaka huu, anza kujipanga sasa kwa semina ya mwaka 2018. Nitatoa taarifa za semina mapema sana na utakuwa na muda wa kutosha kujipanga ili kuhakikisha chochote hakikuzuii kuhudhuria semina hii.

Kwa wale waliohudhuria niliwashirikisha maono yangu makubwa juu ya semina hizi, kwamba tutakuwa tunafanya semina hizi mara moja kila mwaka, na lengo semina ni ziwe za zaidi ya siku moja. Tupate kama siku mbili za kukaa mahali, kujifunza, kushirikiana na kujipanga kiasi kwamba mtu ukitoka hapo unakuwa na moto wa hatari sana. Unatoka ukiwa umeiva, ukiwa una kila kitu cha kukuwezesha kwenda kwa mwaka mzima. Hili litawezekana na tunalifanyia kazi.

Leo sina mengi ya kukuambia rafiki yangu, ndani wa wiki hii nitakushirikisha ratiba kamili ya mwaka wa mafanikio 2017/2018 na jinsi ya kunufaika na mwaka huu wa mafanikio.

Hizi hapa ni picha za matukio mbalimbali ya semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2017.

semina 2017 6
Wanamafanikio wakiwa kwenye semina
semina 2017 5
Mwanamafanikio akiuliza swali
semina 2017 4
Sehemu ya wahudhuriaji wa semina
semina 2017 3
Kocha Makirita Amani akifundisha
semina 2017 2
Mwalimu Felix Maganjila akifundisha
semina 2017 1
Wanamafanikio wakijinyoosha baada ya masomo ya muda mrefu
semina 2017 8
Picha ya pamoja na baadhi ya wanamafanikio
semina 2017 7
Picha ya pamoja na baadhi ya mafanikio

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog