No great thing is created suddenly. – Epictetus
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo mazuri sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ACHA HARAKA…
Ukilima shamba lako vizuri, ukapanda mahindi yako vizuri, yakaanza kuota na ukaweka mbolea, halafu baada ya wiki moja ukaenda na kikapu unataka kuanza kuvuna mahindi, watu wataona una tatizo kubwa.
Watakushangaa sana kwa sababu kulima na kupanda mahindi pekee hakukupi nafasi ya kuvuna, unahitaji pia kuyapa muda, ili yaweze kukua, kuzaa na kukomaa.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye kila kitu tunachofanya kwenye maisha yetu, kila kitu kinahitaji muda.
Utakuwa unaishangaza dunia kama unaanza biashara leo halafu ndani ya mwezi mmoja unataka uanze kuitegemea biashara hiyo moja kwa moja.
Au umeanza kazi, na ndani ya muda mfupi unataka kuwa umeshapata kila unachotaka na umeshajua kila kitu.
Tumekuwa tukijidanganya sana kwenye haya, na tumekuwa tunaishia kuibiwa, kutapeliwa au kupoteza kile tunachotaka.
Kila kitu kinahitaji muda,
Hivyo subira ni muhimu,
Acha haraka.
Juhudi, maarifa kujituma ni muhimu, lakini muda ni muhimu zaidi.
Kila unachotaka kwenye maisha yako, kipe muda.
Ukawe na siku bora sana leo, uwe na subira.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa
Asante dk kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike