KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 87 – 96.
Inakuwaje pale unapokuwa na kitu kizuri ambacho kinaweza kukusaidia lakini hukitumii?
Yaani ni sawa na una fedha zako mwenyewe, za kukutosha, lakini unaenda kuwa ombaomba.
Hivi ndivyo wengi wanavyoishi kwenye maisha hao. Wana vitu ambavyo vingeweza kuwasaidia lakini hawavitumi.
Na sehemu ya vitu hivyo ni milango mitano ya fahamu tuliyonayo.
Milango hiyo ni KUONA, KUSIKIA, KUONJA, KUNUSA NA KUHISI.
Leonardo anasema watu wengi;
đź’Ąwanaangalia lakini hawaoni.
đź’Ąwanasikiliza lakini hawasikii.
đź’Ąwanashika lakini hawahisi.
đź’Ąwanakula nila kuipata ladha.
đź’Ąwanatembea bila kutambua mazingira yanayowazunguka.
đź’Ąwanavuta hewa bila ya kuipata harufu.
đź’Ąwanaongea bila ya kufikiri.
Ukiangalia kwa kina, utaona jinsi gani sehemu kubwa ya maisha ya watu iko hivyo. Hatutumii kabisa milango ya fahamu tuliyonayo.
Leonardo da Vinci aliweza kutumia vizuri milango yakenya fahamu, na hilo lilimwenzesha kuwa mtu mwenye fikra nzuri.
1. Yape macho yako kazi ya kuona, siyo tu kuona kwa nje, bali kuona visivyoonekana (Maono)
2. Yape masikio yako uwezo wa kusikiliza, kusikiliza ili kielewa na siyo kusikiliza ili kujibu au kupinga.
3. Upe ulimi wako nguvu ya kuonja, uonje na kitambua kila aina ya ladha iliyopo kwenye kile unachokula.
4. Ipe pua yako uwezo wa kunusa na kutanbua harufu.
5. Ipe ngozi yako nguvu ya kuwa na hisia kwa kila unachogusa.
Tukitumia vizuri milango yetu ya fahamu, tutaweza kuziona fursa nyingi sana zinazotuzunguka pale ulipo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa