The world turns aside to let any man pass who knows where he is going. – Epictetus
Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari DUNIA ITAKUPISHA KAMA…
Watu wengi wamekuwa wanakwama kwenye mambo wanayotaka kufanya au kupata, kwa sababu dunia inakuwa imewakwamisha.
Ni kweli dunia inaweza kuwa kizuizi na kikwazo, dunia inaweza kukunyima chochote unachotaka.
Lakini pia dunia ipo tayari kukupisha na kukupa chochote unachotaka kama…
💥 Unajua hasa kile unachotaka.
💥 Upo tayari kulipa gharama ili kukipata kitu hicho.
💥 Upo tayari kuvumilia hata kama itachukua muda kukipata.
💥 Hukubali haraka pale unapokutana na kikwazo chochote.
Jua hasa kile unachotaka na kuwa tayari kukipata, na dunia itakupisha ukipate.
Dunia inawazuia na kuwanyanyasa wavivu na wanaokata tamaa mapema.
Lakini inawaogopa wapambanaji na wasiokata tamaa.
Tukaendeleze mapambano leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha
Ahsante ndugu kwatafakari nzuri
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike