Zipo kampuni kubwa sana duniani ambazo zinafanya vizuri sana lakini wakati zinaanza hazikuanza kama hivyo unavyoziona, zilianza kama kitu kidogo sana tena si hivyo tu zilianza zikiwa na mtu mmoja peke yake.

Wapo wana michezo wakubwa sana duniani, ambapo wakati wanaanza kazi huduma zao, hakuna hata mmoja aliyehisi au kutambua kwamba wanaweza wakawa watu wakubwa sana na wenye mafanikio makubwa.

Wapo waandishi nguli wa vitabu, ambao wakati wanaanza kuandika, walikuwa wakiandika neno moja moja kwa mfumo wa kudonoa na kwa siku walikuwa wakiandika maneno machache sana , lakini leo hii ni waandishi wakubwa sana.

Ipo miti mikubwa sana duniani, lakini miti hiyo wakati ina anza haikuanza hivyo, ilianza kama mchicha, lakini leo hii ni miti mikubwa ambapo kuing’oa kwake ni lazima utafute msaada wa vifaa vikubwa pia.

Soma; Mambo Manne (4) Yatakayokuzuia Usikamilishe Kile Unachokifanya.

kuzabiasharaPia yapo majengo makubwa sana, ambayo wakati yana anza kujengwa, yalianza kujengwa kwa msingi na tofali moja moja, lakini baada ya muda ni majengo makubwa na ni marefu sana na kushagaza hata wengi kwamba yalijengwaje.

Kwa mantiki na mifano hiyo, inatuonyesha wazi kila kitu kilichopo dunia kinaweza kikakua na kuleta mafanikio makubwa, ikiwa kitu hicho kitalelewa katika mazingira mazuri ya kuweza kukiruhusu kiweze kukua.

Pasipo kujali kwamba ni elimu, mahusiano, biashara, au kitu chochote kile, lakini uwezo wa kitu hicho kuweza kukua na kuleta mafanikio makubwa, upo tena kwa asilimia zote kabisa na bila shida ikiwa lakini kitalelewa katika mazingira yakuruhusu kikue.

Kumbuka nimesema kila kitu inaweza kukua ikiwemo hata wewe. Unaweza ukawa unajiona umedumaa na huwezi tena kusogea mbele kimafanikio, lakini tu nikwambie ukweli uwezo wa kufanikiwa unaoa tena mkubwa tu.

Haijalishi eti kwa sababu umeanza na kidogo ndio hutaweza kufika mbali, wala haiko hivyo. Popote pale ulipo na chochote kile ulichonacho unaweza ukaanza nacho hichohicho na kikakusaidia kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Soma; Jambo Moja La Uhakika Unalopaswa Kulijua Kuhusu Mafanikio Kwenye Maisha Yako.

Hakuna kizuizi, anza safari yako ya mafanikio makubwa na kuanza na kidogo. Hatua ya mafanikio yako makubwa inaaza na kwa wewe kuchukua hatua hizo ndogo ndogo ambazo wengi wanazidharau sana.

Ikiwa kama wewe utakazana kuchukua hatua kidogo kila siku, itafika wakati hizo zitakuwa sio hatua kidogo tena bali itakuwa ndio safari ya kuelekea kwenye mafanikio yako makubwa inazidi kupamba moto.

Kuanza na kidogo ni jambo zuri sana kuliko kutokuanza kabisa. Kama kuna kitu unataka kukianza usisubiri ujikusanye sana ndio uanze, Najua hatua ya kwanza ni ngumu, lakini kazana na anza na hicho kwanza ulichonacho hadi kufikia mafanikio yako makubwa.

Hakuna kitu ambacho ni kikubwa kilianza kama unavyokiona. Kila kiu kilianza mbali tena kikuwa kidogo sana. Kama iko hivyo kwa nini wewe unataka mafanikio yako yatokee ghafla, kwa nini unatafuta muujiza wa namna hii?

Mambo makubwa siku zote yanapatikana kwa muda. Upo muda wa mafanikio yako unakuja, unachotakiwa kufanya ni kuendelea kuweka juhudi kubwa kila kukicha mpaka uweze kufikia kwenye mafanikio uyatakayo.

Haijaishi upo kwenye biashara gani au huduma gani lakini hapo ndipo mahali pa kuanzia na njia ya mafanikio yako ipo hapo. Usije ukajikatisha tamaa kwa kusema mbona mimi nafanya kazi ya hovyo sana ambayo haiwezi kunisaidia kutoka kimaisha.

Soma; Usiruhusu Sauti Hii Ikakufanya Ukashindwa Kufanikiwa.

Naomba uelewe tu kwmba hapo ulipo ni mwanzo tu. Hiyo ni sehemu kwako ya kuanzia na upo kama kwenye kujifunza. Weka juhudi kubwa kila siku, ili juhudi hizo ziweze kukusaidia kuweza kusonga mbele na kufikia mafanikio makubwa.

Kitu ninachotaka unielewe hapa leo ni kwamba, kwa popote ulipo na chochote unachotaka kukimailisha anza na kidogo ulichonacho, kwa kuanza na kidogo ulichonacho hiyo ndiyo njia kubwa ya kukusaidia kuweza kufikia mafanikio yako.

Fanyia kazi haya, na chukua hatua za kuhakikisha ndoto yako inatumia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http//www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com