Katika mchezo wowote ule, timu ikiingia uwanjani kwa lengo la kushinda, mchezo unakuwa mzuri na watazamaji wanafurahia. Lakini kama timu itaingia uwanjani kwa lengo la kutokushindwa, basi mchezo unakuwa siyo mzuri, burudani inakosekana.
Fikiria kama mchezo ni wa mpira wa miguu, kama timu inacheza ili kushinda, mashambulizi yatakuwa mengi na mchezo unakuwa mzuri. Lakini kama timu inaingia uwanjani kuhakikisha haifungwi, wachezaji wote wakakaa golini ili kuzuia timu isifungwe, mchezo unakosa uzuri wake.

Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya mafanikio.
Kama chochote unachofanya ni kwa ajili ya kutaka kushinda, utapiga hatua kubwa, utaziona fursa nyingi na kuweza kufanya mengi na makubwa. Kwa njia hii utaweza kufanikiwa, na kufurahia yale unayofanya pia.
SOMA; UKURASA WA 701; Thamani Iliyopo Ndani Ya Kushindwa…
Lakini kama chochote unachofanya utakuwa unakwepa kushindwa au kukosea, utashindwa kufanya vitu vingi. Utaogopa kuchukua hatua, utakuwa na hofu kwamba chochote unachofanya kitashindwa. Hapo hutaweza kufanya makubwa na utabaki pale ulipo.
Hivyo ni muhimu sana kuweka mtazamo wetu sawa kwa chochote tunachofanya. Tuache kukimbia kushindwa na kukosea na tuanze kukimbilia kushinda na kupiga hatua.
Ushindi unakujwa kwa kupambana ili kupiga hatua na siyo kukwepa kuchukua hatua. Mafanikio pia yapo kwenye hatua unazochukua na siyo hatua unazokwepa kuchukua.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog