Habari za leo rafiki yangu?

Karibu tena kwenye utaratibu wetu wa kitabu cha mwezi, ambapo kila mwezi nimekuwa napendekeza kitabu kimoja kwa marafiki zangu kukisoma, ambacho kitawasaidia kupiga hatua kwenye maisha yao na kufanikiwa zaidi.

Kumekuwa na dhana kwamba watu wengi hasa sisi waafrika siyo wasomaji wa vitabu. Ipo mpaka misemo kwamba ukitaka kumficha mwafrika kitu, kiweke kwenye maandishi.

Ni kweli kwamba maarifa mengi sana yapo kwenye vitabu. Magumu na changamoto ambazo watu wengi wanapitia, zina majibu kwenye vitabu mbalimbali vilivyoandikwa. Lakini wengi wanashindwa kuyapata kwa sababu hawana mfumo mzuri wa kusoma vitabu.

Baada ya kufanya utafiti kwa wengi, kwa nini hawasomi vitabu, changamoto kubwa zimekuwa ni mbili; kukosa muda wa kusoma vitabu na kukosa vitabu vya kusoma.

Baada ya kuona changamoto hizi, nikaandaa program maalumu ya kutatua changamoto hizi mbili. Programu hii inaitwa KURASA KUMI ZA KITABU.

Kwenye program hii kila siku mtu unasoma kurasa kumi za kitabu, kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya hata kama amebanwa kiasi gani. Pia kwenye program hii napendekeza vitabu vya kusoma na kutoa baadhi ya vitabu ambavyo watu wanaweza kusoma.

Kujiunga na program hii unalipa ada ambayo ni tsh 10,000/= kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha unatuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenye moja ya namna hizo na unapata nafasi ya kuingia kwenye program hii.

Mwezi disemba 2017 napendekeza marafiki zangu wote wasome kitabu THINK AND GROW RICH.

think and grow rich

Think and grow rich ndiyo kitabu cha kwanza kabisa katika zama hizi za harakati za maendeleo binafsi ambacho kinatoa mwongozo wa namna ya kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha.

Hichi ni kitabu ambacho kilitokana na utafiti uliofanywa kwa miaka 25 kwa watu zaidi ya 500 waliokuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Kitabu hichi kimeandikwa kutokana na mifano halisi ya namna watu walivyoishi na kufanya mambo yao.

Naweza kusema vitabu vingi vya mafanikio na maendeleo binafsi, vina msingi wake kwenye kitabu THINK AND GROW RICH. Kitabu hichi kina falsafa kamili ya mafanikio ambapo kuna misingi 16 ya kuweza kufanikiwa kwenye maisha.

Kupitia kitabu hichi, unajifunza umuhimu na nguvu ya mawazo yako katika kukufikisha kule unakotaka. Kitabu hichi kitakufungua kuweza kujijua wewe mwenyewe na kuziona fursa nyingi ambazo tayari zinakuzunguka hapo juu.

Kwenye kitabu hichi, utajifunza pia kwa watu waliokata tamaa wakiwa wameyakaribia kabisa mafanikio yao. Hili litakufanya usikate tamaa kamwe kwenye maisha yako. Kwa sababu mambo yanapokuwa magumu, unakuwa umekaribia ushindi wako.

Kama utasoma kurasa kumi kila siku za kitabu hichi, basi ndani ya mwezi huu wa 12 utamaliza kitabu hichi. Na muhimu zaidi utaondoka na mambo ya kufanyia kazi ili maisha yako yawe bora zaidi ya yalivyo sasa.

Nakusihi sana rafiki yangu soma kitabu hichi, hata kama ulishakisoma, kisome tena, kitakusaidia mno. Kurudia kusoma kitabu unajifunza mengi zaidi.

Kama una kitabu hichi kisome, kama huna karibu kwenye program ya KURASA KUMI ZA KITABU na utapata kitabu hichi pamoja na mwongozo mzuri wa kukisoma ndani ya mwezi huu.

Kujiunga na program ya KURASA KUMI ZA KITABU lipa ada ambayo ni tsh 10,000/= kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe kwa njia ya wasap na utaunganishwa.

Usomaji

Nakutakia kila la kheri kwa mwezi huu mpya wa disemba 2017, mwezi wa mwisho kwa mwaka 2018. Nenda ukajifunze makubwa, ufanye makubwa na kupiga hatua kubwa za kuelekea kwenye mafanikio yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog