3413; Kutaka na Kupata.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kupata chochote kile unachotaka,
Ni lazima ukitake hasa,
Uwe tayari kulipa gharama ya kukipata,
Na uwe na subira kwenye kukipata.

Wote wanaokosa yale wanayotaka,
Ni kwa sababu hawakutaka hasa kupata,
Hawakuwa tayari kulipa gharama ya kukipata,
Na wanakuwa na haraka sana ya kukipata.

Kama hujapata chochote unachotaka, angalia maeneo hayo matatu.
Je hicho ndiyo kitu ambacho unakitaka hasa? Je ndiyo kipaumbele cha kwanza kabisa kwako?
Kama siyo, ni bora uendelee na mengine, kwa sababu huwezi kupata kile ambacho siyo kipaumbele cha kwanza kwako.

Jiulize pia ni gharama gani ambazo tayari umezilipa kwenye kupata unachotaka.
Ni kazi kubwa kiasi gani ambayo tayari umeashaiweka kwenye hicho unachotaka?
Ni yapi nazuri ambayo umeyakosa kwa sababu ya kupambania kupata unachotaka?

Na mwisho jiulize umeshakaa kwenye mapambano hayo kwa muda mrefu kiasi gani.
Kama umekuwa mtu  wa kuruka ruka na vitu  vingi ili kutafuta urahisi, huwezi kupata unachotaka.
Pamoja na juhudi kubwa unazokuwa unaweka, kuna swala la muda pia.
Wakati mwingine kinachokuwa kinahitajika ni muda.
Endelea na kitu chako mpaka pale umekipata.

Hakikisha hukosi chochote unachotaka kwa kuzingatia haya uliyojifunza hapa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe