As long as you live, keep learning how to live. – Lucius Annaeus Seneca

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio ni TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo mwaka huu 2018 tunakwenda kufanya makubwa.

Asubuhi ya leo tutafakari KILA SIKU NI DARASA…
Kila siku ya maisha yetu ni darasa,
Hii ni kwa sababu kwenye kila siku kipo kitu ambacho tunajifunza, iwe ni kitu kipya kabisa ambacho ndiyo tunakijua au kitu ambacho tayari tulikiwa tunakijua na kusisitiziwa zaidi.

Hakuna siku inayopita ambayo haitupi kitu cha kujifunza au kutusisitizia kitu ambacho tayari tulishakijua.
Hivyo ni wajibi wetu kuchukulia kila siku kwa uzito wake, kuhakikisha tunajifunza kweli ili kuweza kupiga hatua.

Kitu kikubwa zaidi ambacho tunajifunza kila siku, ni jinsi ya kuishi vizuri. Hakuna aliyebobea kwenye hilo na hivyo ni zoezi ambalo tunapaswa kufanya kila siku.
Hivyo mwanamafanikio, kama bado upo hai, basi jua jukumu lako la kwanza ni kujifunza kuishi vizuri.

Twende tukajifunze kupitia maisha leo, twende tukajifunze jinsi ya kuisho vizuri leo.
Na siku hii ikawe njema sana kwa kila mmoja wetu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha