Time is a sort of river of passing events, and strong is its current; no sooner is a thing brought to sight than it is swept by and another takes its place, and this too will be swept away. – Marcus Aurelius
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.
Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NA HILI LITAPITA…
Muda ni tiba nzuri ya kila jambo,
Hata kama unapita kwenye wakati mgumu kiasi gani,
Hata kama unapitia changamoto gani,
Kitu kimoja unachopaswa kujua ni kwamba, kila kitu kinapita.
Muda wa maisha yetu ni kama mto unaotiririka maji,
Matukio tunayokutana nayo ni sawa na mawimbi ya maji.
Ambayo yanakuja na kupita haraka, na kufuatiwa na mawimbi mengine.
Hivyo chochote unachopitia sasa, au utakachopitia kwa wakati wowote, kitapita.
Lakini kikipita, kinaweza kukuacha ukiwa imara zaidi au ukiwa dhaifu zaidi.
Kitakuacha imara kama utakifanyia kazi, na kitakuacha dhaifu kama utakikwepa na kukikimbia.
Na hakuna sababu yoyote ya kukimbia kile kinachopita,
Ni vyema kutenga muda wa kukifanyia kazi, ili kinapopita kikuache ukiwa imara, na chochote kinachokuja kikukute uko imara zaidi.
Chochote unachopitia, hata kama ni kigumu kiasi gani, au kizuri kiasi gani, jua kipo kwa muda tu, kinapita.
Hivyo ni wajibu wako kuchukua hatua wakati kitu kipo na hakijapita bado.
Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha