“The best day of your life is the one on which you decide your life is your own. No apologies or excuses. No one to lean on, rely on, or blame. The gift is yours – it is an amazing journey – and you alone are responsible for the quality of it. This is the day your life really begins.” – Bob Moawad
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2018, ambao unatuwezesha kufanya makubwa zaidi.
Asubuhi ya leo tutafakari SIKU UNAYOANZA KUISHI…
Wapo watu ambao wanaishi maisha hao, wachache,
Na wapo watu ambao wanasukuma siku zisogee, wengi sana.
Tofauti kubwa kati ya watu hao wawili inaanzia kwenye kiwango cha majukumu ambayo mtu anayakubali.
Wale wanaoishi maisha, wanakuwa wamekubali na kubeba majukumu yote ya maisha yao. Hutawakuta wakilalamika au kulaumu kwamba watu wengine ndiyo kikwazo kwao. Hutawasikia waitoa sababu yoyte ile kwa nini hawajapata wanachotaka, au kwa nini wameshindwa kwenye kitu fulani.
Watu hawa wanajua maisha yao ni jukumu lao, chochote kinachotokea au kutokutokea ni kwa sababu zao wenyewe. Wanajua hakuna yeyote anayekosa usingizi kwa wababu ya maisha yao, na hivyo wanachukua kila hatua kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora zaidi.
Wale wanaoigiza maisha sas, ni watu ambao wamevurugwa sana na maisha yao.
Ni watu ambao wana kila mtu na kila kitu cha kulaumu na kulalamikia kwa nini maisha yao siyo mazuri.
Watakupa kila ina ya sababu kwa nini hawajapata wanachotaka au kushindwa.
Ni watu ambao kila wakati utawakuta wakitafuta njia ya kutoroka matatizo yao badala ya kuyatatua.
Swali ni je, wewe unaishi maisha yako au unaigiza maisha?
Kabla hujakimbilia kusema unaishi maisha, kwa kuwa unajiambia hulaumu yeyote, nikupe mfano huu.
Ikitokea unapita barabarani, pembeni kabisa, sehemu ya watembea kwa miguu, na ghafla bila hata ya kujua unashanga gari imetokea kusikojulikana na imekugonga na ukaumia. Unafikiri nani anapaswa kulaumiwa?
Kwa fikra za haraka ni dereva wa gari kwa nini amekuja kukufuata kwenye njia ya waenda kwa miguu.
Na hicho ni kielelezo tosha kwamba hujaanza kuishi maisha yako.
Kama umeanza kuishi maisha yako wa kulaumiwa ni wewe,
Kwa nini ulipita kwenye njia hiyo na kwa wakati huo?
Kwa nini hukiwahi zaidi?
Kwa nini hukuwa na umakini zaidi wa kuweza kuona hatari inayoweza kujitokeza?
Yapo mengi ya kuonesha wa kulaumiwa ni wewe mwenyewe na hivyo unachopaswa kufanya ni kujifunza na kuchukua hatua.
Kama utajiaminisha kosa siyo lako, hujaanza kuishi maisha.
Sasa jiulize vizuri zaidi, unaishi maisha au unaigiza maisha?
Pata jibu sahihi kisha chukua hatua.
Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha